IBADA YA SHUKURANI NDANI YA BCIC MBAGALA MAJI MEUPE


Wengi huwa tunaomba na kusahau kwamba kwenye kwenye kushukuru kuna utimilifu wa kila jambo. Wale wakoma kumi walioponywa, ni mmoja wao tu alirudi kumshukuru BWANA Yesu, na hakika katika kufanya hivyo akaambiwa...

Mama Askofu Michael Imani
Katika kutazamia hilo, ndio maana BCIC Mbagala Maji Meupe wameandaa ibada ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya kufika 2015 yenye ahadi za baraka tele kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi jioni. Uje wewe pamoja na wenzako kwa ajili ya kumshukuru Mungu maana tayari timu ya kusifu na kuabudu imeshakaa sawia kwa ajili ya kushusha uwepo wake. Joyce Matenge kutoka Kenya atakuwa akishirikiana na timu ya kusifu na kuabudu live.

Sarah K tayari yuko ndani ya nyumba kwa ajili ya kushirikiana na waimbaji wengine wa hapa nchini ambapo mambo yote yatakuwa murua. Upendo Nkone atakuwepo pia kuhakikisha utukufu kamili unashuka.

Namna ya kufika yakupasa upande mabasi ya Mbagala na kutokea hapo upande mabasi ya kwenda Mbande ama Chamazi. Kanisa linaitwa BCIC Maji Meupe kwa Askofu Michael Imani.

Tuatukuletea puicha zaidi za tukio hili kama lilivyokuwa studio.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.