JE, WAJUA KUWA MAPEPO NI HATARI SANA?

Picha mfano wa pepo©dreamatico

JE, WAJUA KUWA MAPEPO NI HATARI SANA?

Ugomvi mkubwa kati ya mabinti mawili ulikusanya umati mkubwa wa watu. Binti mmoja alikuwa anataka kumuua mwenzake kwa kisu kikubwa aliyekuwa akimtuhumu kwa mambo fulani. Tukio lile lilikuwa limepelekwa mbele ili hatua za kisheria zichukuliwe jambo ambalo lilihatarisha ajira ya yule binti na ndoa ya binti mwingine ilikuwa hatarini.

Aliyeshughulikia jambo lile kijamii alipewa taarifa zangu na alihitaji ushauri wangu nami nikaomba nionane na wahusika. Wale mabinti waliitwa kwa kuwa yule aliyekuwa analishughulikia alikuwa na mamlaka fulani juu yao. Niliwahoji maswali machache wahusika na nikiwa naendelea nao, nikasikia msukumo wa kutaka kuomba na kuweka mikono juu ya mmoja wao.

Nilimuomba yule ndugu aniruhusu nifanye maombi na akanikubalia. Ghafla, binti aliyetishia kuua alianza kupiga kelele na kulia kwa sauti kuu ikiwa ni ishara ya kupagawa na mapepo. Ilichukua zaidi ya nusu saa kwa yule binti kufunguliwa. Mara ya baada ya kufunguliwa, uchungu uliokuwa umemjaa moyoni yule binti ukamtoka na akajawa na furaha kuu moyoni na akamuomba msamaha mwenzake. Kwa kuwa yule aliyekuwa anashughulikia lile jambo alikuwa ni Muislam, alishangaa sana kuona kuwa kumbe mtu aliyepagawa na mapepo anaweza hata kuua pasipo kujitambua.

Panapo Majaliwa!
Mch. Emmaus Bandekile Mwamakula
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.