KWA TAARIFA YAKO: KUVUNJIKA KWA NDOA MBILI KULIVYOHARIBU HUDUMA YA MWIMBAJI NYOTA AFRIKA YA KUSINI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nchini Afrika ya kusini ambako tunakujuza japo kwa ufupi tu madhara ya misukosuko ya ndoa kwa watumishi wa Mungu namna inavyopokelewa na watu waliokuwa wakiwasapoti na kuipenda huduma ya watumishi hao. Leo ni kuhusiana na mwimbaji maarufu zao la kundi la Joyous Celebration mwimbaji mtume na mchungaji Kekeletso Phoofolo ama kwa kifupi mwite Keke lenye maana ya ongezeka 

KWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyu amevuma sana nchini kwake Afrika ya kusini na kutokea kupendwa sana hasa kupitia huduma yake ya uimbaji binafsi na kupitia wimbo wake wa Che che che, amefahamika akiwa na Joyous bila kusahau Spirit of Praise pamoja na waimbaji wengine binafsi alioshirikiana nao. Lakini alipata pigo kubwa sana katika huduma pale aliporuhusu ndoa yake ya pili na mwanadada Mpho kuvunjika na kupeana naye talaka huku wakiwa wamepata mtoto mmoja katika ndoa yake hiyo na kufanya mtumishi huyo kuwa na jumla ya watoto watatu kwakuwa katika ndoa yake ya kwanza alibarikiwa kupata watoto wawili.


Keke na watoto wake kushoto ni Lesedi na kulia kwake ni Kganya ©Keke


KWA TAARIFA YAKO kitendo cha mwimbaji huyu kuachana na mkewe wa pili kilimpa wakati mgumu sana hata kuamua kuhama kanisa alilokuwa akilitumikia kwa miaka takribani nane la Shekinah Glory Worship Tabernacle na mpango wake ukiwa kuhamishia huduma yake eneo lingine lijulikanalo kama Tshwane huko huko Afrika ya kusini huku pia taarifa zikisema mtumishi huyo ambaye alikuja nchini Tanzania mwaka jana wakati wa tamasha la Pasaka anampango wa kuoa mke mpya ambaye atafanya kuwa na jumla ya kufunga ndoa tatu mbili zikiwa zimeshindikana baada ya kuachana na wake zake.

KWA TAARIFA YAKO kisa cha mwimbaji huyo kushindwa katika ndoa zake mbili ni kwamba inadaiwa ana hasira za karibu sana hali inayosababisha kufikia kumpiga mkewe na vitendo hivyo huwa
Keke na mkewe wa pili Mpho wakati mjamzito
vya mda mrefu na kusababisha wake zake kumkimbia. Keke amewahi kukaririwa akisema hafurahishwi na vitendo anavyofanya na anajitahidi kupambana navyo ili visiwe sehemu ya maisha yake na kuwataka watu wote kuwaombea sana watumishi kwakuwa wengi wao hawapendi kuwa na mapangufu hayo ila inajitokeza kwakuwa wao pia ni binadamu kama walivyo binadamu wengine.
KWA TAARIFA YAKO Keke kama ilivyo kwa mwimbaji mwingine nyota kijana Lundi Tymara, pia nayeye kabla ya kutoa album mbili za gospel kwa mafanikio ikiwa pamoja na kuongoza vipindi viwili vya gospel kwenye runinga aligubikwa na utumiaji wa madawa ya kulevya pamoja na pombe kali, na kwamba alipoachana na mkewe wa kwanza haikuandikwa sana kwenye vyombo vya habari kwakuwa hakuwa anafahamika sana ila alipoachana na mkewe wa pili hali ilikuwa mbaya hata kufikia watu kuto mwalika katika huduma zao na yeye pia huduma yake kuyumba huku yeye mwenyewe akikiri kwamba mkewe wa pili alifanyika baraka katika maisha yake kwa ujumla.
KWA TAARIFA YAKO Keke amepitia maisha ya watoto wa mitaani kwakuishi geto ndiko alikopata tabia zote zinazotajwa za yeye kujihusisha na mambo ya madawa ya kulevya pamoja na utumiaji wa pombe kali ambazo kwasasa anamshukuru Mungu kwamba ameweza kupambana na matatizo hayo na tayari Mungu amemvusha salama, zaidi amewasihi waumini ama wafuasi wa Kristo kusimama kwaajili ya kuwaombea watumishi wao kwakuwa wanapitia majaribu mazito katika huduma zao. Baada ya kimya cha muda mrefu kutokana na kusongwa na matatizo ya kuvunjika kwa ndoa yake, mwimbaji huyo ameanza kurejea tena kwa kishindo baada ya kutambulisha kati ya nyimbo zake mpya wakati wa kipindi alichofanya kwenye runinga cha gospel time siku ya jumapili iliyoisha.


Keke akiwa na mtoto wake wa kwanza aitwaye Kganya, wanafanana sana©Keke

Silas Mbise wa GK katikati akiwa pamoja na Keke kuume pamoja na Hudson wakati mwimbaji huyo alipotembelea studio za WAPO Fm Radio mwaka jana maalumu kwa tamasha la pasaka
Binti yake Keke, Azania Naledi aliyempata katika ndoa yake ya pili©Keke
Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO vinginevyo tukutane wiki ijayo…..
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.