KWA TAARIFA YAKO: LEAH MOUDDY WA BONGO STAR SEARCH AAMUA KUREJEA KANISANI KUMSIFU MUNGU

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Tangazo la onyesho lililoandaliwa na Leah mwaka jana November

KWA TAARIFA YAKO hii leo ni kuhusiana na mwimbaji aliyetokea kuwika sana wakati wa kinyang'anyiro cha shindano la Bongo Star Search (BSS) ya kwanza ambayo mshindi wake alikuwa mwanakaka Jumanne Idd ambaye hata hivyo hatujui kama bado yupo kwenye muziki au alistaafu. Tuachane na huyo mtu ambaye tunamzungumzia japo kidogo si mwingine bali ni mwanadada Leah Mouddy ambaye aliweza kuwika haswa kupitia shindano hilo na wengi kumtabiria kushinda lakini akaishia kushika namba mbili.

KWA TAARIFA YAKO Leah alikuwa mmoja wa wanakwaya wa kwaya ya Vijana Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam, ambako alikuwa akituma sauti yake kumsifu Mungu pamoja na wenzake ambao nao pia wamejaaliwa vipaji vya uimbaji. Leah ameshiriki na kwaya hiyo kwa kipindi kirefu ikiwa pamoja na kurekodi kanda na kwaya hiyo ambayo hupata mwaliko ubalozi wa Marekani kila mwaka katika kuimba hususani siku ya kuadhimisha uhuru wa nchi hiyo.


Baadhi ya waimbaji wa kwaya ya Vijana Kijitonyama wakiongozwa na Star Munisy mbele.
KWA TAARIFA YAKO Leah aliacha kwaya na kujikita kwenye muziki wa dunia mara baada ya kuachana na BSS na kujifungua mtoto wake haswa ikikumbukwa kwamba wakati anashiriki kinyang'anyiro hicho alikuwa mjamzito. Baada ya kuwa nje ya muziki wa kanisani kwa kipindi kirefu ni kwamba Leah ameamua kurejea tena kanisani kumuimbia Mungu wake ambapo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana Leah aliandaa tamasha maalumu la kusifu na kuabudu akiwashirikisha waimbaji mbalimbali bila kumsahau mmoja kati ya waimbaji nyota wa kwaya ya Vijana Kijitonyama ambaye pia ni mwanzishaji wa nyimbo wa kwaya hiyo Stella Munisi ama mwite Star Munisy ambaye pia hivi karibuni anatarajiwa kuachia video ya album yake ya kwanza.
KWA TAARIFA YAKO kuna mengi ya kungojewa kwa hamu kutoka kwa mwimbaji huyu ambaye amejaliwa sauti nzuri katika uimbaji. GK itakupatia taarifa zaidi ya maendeleo yake katika kuliinua jina la BWANA kupitia huduma za kanda na mialiko pale tutakapoipata. Vinginevyo hii ndio KWA TAARIFA YAKO hii leo, tukutane tena wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.