KWA TAARIFA YAKO: MUIGIZAJI HOLLYWOOD ALIYEPANIA KUMTANGAZA MUNGU KINAMNA YAKE

Tyler Perry kwa nyakati tofauti kazini.
Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Kwa wale watazamaji wa filamu za Tyler Perry, hakika watakuwa wanafahamu filamu za mwanamama mwenye vituko visivyokauka, Madea. Filamu mojawapo ambayo inafahamika fika na mamilioni ya watu ulimwenguni kote ni Madea goes to jail.

Uzuri wa fikamu hii si tu kwamba imesheheni vituko, bali imeigizwa na Tyler Perry. Muandaaji na muongozaji wa filamu ambaye lengo hasa za filamu zake, ameeleza kutaka kugusa maisha ya watu mwa namna ya kipekee, ili basi nao wapate kumgeukia Mungu, ambaye anafanya makuu kwenye maisha yake.

Pamoja na uhusika wa Madea kuwa na ukorofi wa kila namna. KWA TAARIFA YAKO Tyler amekiri kwamba ni kweli Madea si mkristo, na wala hawezi kuwa, ila kuna watu huwa wanavutiwa na matendo yake, hivyo wao huja kumuona na tabia zake, kwa mfumo huo basi anatumia wahusika wengine tofauti na Tyler kufikisha ujumbe anaohitaji uifikie jamii, hapo ndio mwanzo wa mafanikio yake.

Kwa nyakati tofauti Tyler amekuwa mzungumzaji mzuri kwa wale waliovunjika moyo, ambapo pia kwenye suala la uhubiri hayuko mbali. KWA TAARIFA YAKO tukio lililowahi kuvuta hisia za wengi ni pake alipomuwekea mikono Askofu T.D Jakes, na kuwafanya watu wakubali kwamba Mungu anatumia vyombo vyake kwa kadri apendavyo mwenyewe. (bofya hapa kutazama video ya tukio hili)
Askofu T.D Jakes akiombewa na muigizaji Tyler Perry. ©fb/TD Jakes Ministries
Tofauti na kwa waongozaji wengine ambao mara nyingi huepuka kutumia jina la Yesu ama kumkubali
Mungu, KWA TAARIFA YAKO Tyler anasema kwamba yeye hahofii kwenye filamu yake muhusika akikiri kwamba ni Mkristo, ama anampenda Mungu, kwa kuwa kuna watu wanawakilishwa kwelikweli.

Jina la Tyler Perry limekuwa maarufu Hollywood kutokana na mtazamo wake kuhusu mfumo wa malezi kwenye familia, akiwekea mkazo tabia njema kwa namna tofauti tofauti.

Hiyo ndiyo kwa taarifa yako, vinginevyo tukutane wiki ijayo.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.