KWA TAARIFA YAKO: RAIS WA UFILIPINO AWA MPAMBE WA HARUSI YA WAIGIZAJI MARIMAR NA SERGIO

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo nchini Ufilipino ambako kama ilivyoada huwa tunakupatia matukio makubwa yanayofanywa na waigizaji waliojipatia umaarufu nchini Tanzania na kwingineko kutokana na uigizaji wao hodari kwenye tamthilia mbalimbali ambazo zimekuwa zikirushwa na vituo tofauti nchini, lakini kubwa zaidi kwanini GK inaandika habari zao ni kwasababu waigizaji hawa humtanguliza Mungu mbele na ni waumini wazuri na hukiri jina la Yesu wanapokuwa mahali popote nchini kwao. 

KWA TAARIFA YAKO hapana shaka umewahi kutazama tamthilia ya Marimar iliyowahi kuonyeshwa na kituo cha runinga cha StarTV nchini, sasa waigizaji wakuu wa tamthilia hiyo mwanadada Marian Rivera ama Marimari pamoja na mwanakaka Dingdong Dantes ama Sergio walifunga pingu za maisha ama harusi ya ukweli sio ya maigizo siku ya jumanne wiki hii harusi ambayo ilipambwa na waigizaji mbalimbali waliowasimamia maharusi hao lakini kubwa kuliko ambalo halijawahi kushuhudiwa ni mpambe mkuu wa bwana harusi nafasi ilisimamiwa na Rais wa sasa wa Ufilipino mheshimiwa  Benigno Noynoy Aquino.
KWA TAARIFA YAKO si Rais Aquino tu aliyehudhuria kama msimamizi wa heshima katika harusi hiyo pia dada yake aitwaye Kris Aquino ambaye pia ni mtangazaji maarufu wa runinga na muigizaji wa filamu na tamthilia kama alivyoonekana katika tamthilia ya Hiram (Stolen Moments) iliyoonyeshwa na TVT ama TBC inavyofahamika kwasasa akitumia jina la Diana. Kris inawezekana ndiye aliyetoa jibu haswa la kwanini kaka yake kama Rais wa nchi alikuwa msimamizi wa heshima ama mpambe nayeye akiwemo ndani yake kwani baada ya harusi mwanadada huyo ambaye kwa bahati mbaya ndoa yake ilivunjika hivi karibuni, aliandika kwenye anuani yake ya Instagram kwamba familia yao itaendelea kuwa na moyo wa shukrani kwa waigizaji hao kutokana na mchango wao mkubwa wakati wa kampeni za urais mwaka 2010.

KWA TAARIFA YAKO harusi ya waigizaji hao ambao wanatokea kituo pinzani na ABS-CBN cha GMA network ambacho tamthilia zake hazijasambaa sana zaidi ya Marimar huku ABS CBN inafahamika zaidi duniani kwa tamthilia zake kama The Promise, The long wait, Maraclara na nyinginezo kikiwa na waigizaji kama Angelo, Yna, Maraclara na wengineo ilifanyika katika kanisa Kuu Katoliki la mtakatifu Immaculate huko Cubao ndani ya jiji la Quezon nchini Ufilipino. Harusi hii imekuwa maarufu hata kutangazwa na vyombo mbalimbali vya kimataifa kikiwemo kituo cha ABC cha nchini Marekani ambao walizungumzia ama kustajabishwa na ukubwa wa keki ya harusi ambayo kuna uwezekano kwamba imeingia kwenye kitabu cha Guinness kwa kuvunja rekodi ya kuwa keki kubwa kuwahi kutengenezwa kwaajili ya harusi tu.
KWA TAARIFA YAKO waigizaji hawa wanathaminiwa sana na kituo chao cha runinga cha GMA network hadi kufikia kuitwa malkia na mfalme wa tamthilia kwa kituo hicho ambapo kuonyesha kuwathamini ndani ya tovuti ya kampuni hiyo kuna ukurasa maalumu wa harusi ya Marian na Dingdong bonyeza hapa . Harusi yao ilitumia gharama kubwa kuanzia maandalizi hadi kufanyika kwa harusi yenyewe huku ikielezwa kwamba ni harusi ya mwaka kwa nchini humo kutokana na jinsi ilivyofanyika ikifananishwa na harusi ya ukoo wa kifalme Uingereza.


Maharusi wakila keki yao ambayo ukubwa wake ilisababisha kusafirishwa na watu wasiopungua kumi.
Ndani ya kanisa kuu katoliki la mtakatifu Immaculate Quezon city.
Rais Aquino na bwana harusi wakizungumza kwa furaha kanisani wakati wakimsubiri bibi harusi
Bwana harusi na mpambe wake Rais Aquino wakizungumza mawili matatu 
Bwana harusi akiwa anamsubiri bi harusi wake pembeni ni Rais Aquino
Marian akiwa na wazazi wake, baba yake ni raia wa Uhispania (Spain)
Marian akiingia mbele kukutana na Dingdong
Tayari kwa ndoa
Maharusi wakiwa na nyuso za furaha madhabahuni
Rais Aquino akiwapa pongezi maharusi
Wameshaunganishwa pamoja
Rais Aquino na maharusi
Mkwe wa mwigizaji nyota Yna Macspac ama Kristine Hermosa bwana Vic Sotto ambaye alikuwa mmoja wa wadhamini wa ndoa hiyo akiwa pamoja na dada wa Rais wa Ufilipino bi Kris Aquino katika harusi hiyo.


Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo, tukutane wiki ijayo  HERI YA MWAKA MPYA 2015

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.