MASWALI 7 YATAKAYOKUSAIDIA KUTAMBUA IWAPO INAWAHESHIMU WAZAZI WAKO

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

©Parenting Class
Aina ya maswali unaojuuliza kila siku yanaweza kukusaidia kujua iwapo unasonga mbele au bado uko pale pale siku zote.Aina ya maswali unaojiuliza kila siku yaonyesha ubora wa mawazo ulio nao ndani mwako na muelekoo wa maisha yako.Maswali unaojiuliza kila siku ni moja ya kipimo ambacho kinaweza kukujulisha kwamba upo kwenye season mpya ya maisha yako au bado uko pale pale.Ukiona swali moja unajiuliza kila mwaka au kila siku basi tambua bado hilo eneo haujavuka.

Maswali kila mtu anayojiuliza hutofautiana Ubora ,Maswali yanye Ubora hutoa matokeo bora kila hatua ya kipindi fulani kwenye maisha ya binadamu.Ndio maana utaona Research haziishi kila siku maana yake Research Moja huza maswali ya Research ijayo ambayo huboresha hatua iliyopita.Hakikisha Unaboresha Ubora wa Maswali Unayojiuliza kila Siku ili kuboresha maisha yako.Tukitaka kujua miaka mitano ijayo utakua wapi tunaangalia aina ya maswali unayojiuliza leo.

“Maisha yamejengwa kwenye mfumo wa Maswali, Maswali ni Maisha, Maisha ni Maswali”.

Unapopata majibu ya maswali yalioyopita ,unakuwa umeboresha maisha yako kwa sehemu ambapo Majibu ya Maswali Uliyojiuliza huzaa maswali mengine.

Kwenye Maisha yetu ya kila siku kuna watu ambao tumepewa kuwa Wazazi Wetu hakuna mtu aliyechagua wazazi ambao Mungu amsebabisha kupitia wao tupate Uhai na Kufanikiwa hapa Ulimwenguni.Vitabu Mbali Mbali vya Dini vimetuelekeza Twaheshimu Wazazi wetu ili Maisha yetu yawe marefu na tufanikiwe,Kwa kifupi ni kwamba iwapo maisha yako hayajawa marefu maana yake kuna sehemu Uliwakosea wazazi au haukutekeleza Sheria na Taratibu za Mungu hapa Duniani.Je ni kweli tunawaheshimu Kulingana na Vitabu Hivyo? Maswali Machache yajayo yaweza kukusaidia kujua Iwapo Unawaheshimu Wazazi au Unaigiza kuwaheshimu tu?


(I) Je Kipi ni Kiwango Cha Ukweli Kwenye Mambo Yote Kwa Wazazi Wako?

Moja Ya Kitu ambacho unaweza kujua namna unavyomuheshimu Mtu ni kiwango chako cha Ukweli juu ya mtu huyo,haijalishi anajua kwamba umemdanganya au ume mwambia ukweli.Wewe unayemweleza kitu husika ndio Unajua kwamba unasema ukweli kwa kiasi gani au unadanganya kwa kiasi gani.Mfano tukienda kwa Mungu kumuomba mbali mbali hatumdanganyi kitu chochote sababu tunamuheshimu.Ukiona unamdanganya mpaka Mungu ujue una matatizo yaliyopitiza.Mungu alipokuwa anasema tuwaheshi Wazazi wetu alitaka tuwe wakweli kwa namna zote sio tunakuwa wakweli kwenye eneo moja lakini tunakuwa waongo kwenye eneo lingine kwenye maisha yako.

Maisha yapo kwene mfumo wa kile ulichopanda ndicho Unachovuna,Iwapo unajua kwamba Ulimdanganya Mzazi wako kwa sehemu moja au nyingine rudi nenda katubu na mweleze ukweli wote haijalishi yeye aligundua uongo uliomweleza au hakugundua.Hii unafanya kwa faida yako ili siku zako za kuishi zisipungue na ufanikiwe pia.Mara nyingi Utagundua Wazazi wengi hawatambui kwanini watoto wao ni waongo kumbe tatizo halikuanzia kwa Watoto bali lilianzia kwao wenyewe kwa Kuwadanganya wazazi wao na hawakwenda kutubu ili kufuta hilo tatizo ,Matokeo yake linakuwa kizazi hata kizazi.

“Kiwango cha Ukweli kitakujulisha Kwamba Unawaheshimu Wazazi sawa sawa na Maelekezo ya Mungu au Unaigiza”.


(II) Je Una Muitikio wa Namna gani pale Ambapo Wazazi Wako Wanapokuambia Jambo?
 
Kwa Miaka kadhaa nimekutana na watu kadhaa na marafiki pia wakiwemo moja ya Kauli ambayo nimekuwa nikisikia Mama kazidi kuomba hela au Baba naye kazidi sana.Je upi ni muitikio wako wazazi wanapokuambia jambo hata kama hawakuoni? Fikiria Binafsi Mungu akutokee leo Usiku akuambie nataka kitu fulani Je utamwambia Mungu na wewe umezi kuomba omba? Au Mfano angekua anaongea na wewe kwenye Simu Ungemkatia Simu Sababu kila siku anakueleza Shida zake? AU Ungekuwa unambinulia mdomo kama unavyofanya kwa wazazi wako au sababu hawakuoni? Je Ungekuwa unamlalamikia kama unavyowalalamikia wazazi wako?
Muitikio wako unaonyesha kiwango cha heshima ulicho nacho juu ya wazazi wako.Jifunze kuwa na muitikio halisi na mzuri kwa wazazi wako haijalishi unaloambiwa linakuumiza au hapana .Amri za Mungu zinasema tuwaheshimu.Mbona imekuwa Rahisi kuwaheshimu Mabosi wetu ofisini au sababu wanatupatia Mishahara?Ili Maisha yako yawe Marefu na Mafanikio Badilisha muuitiko wako,Ili kuheshimu wazazi wako.

“Kumbuka aliyetoa amri hii sio Binadamu ni Mungu”

(III) Je Unatabia ya Kuwakosoa Kosoa /Kawarekebisha Wazazi Wako?


“Mungu alipokuwa anaweweka wazazi juu yetu ni kwamba lazima wawe na Mamlaka juu yetu”.

Moja ya Kosa ambalo tunafanya kizazi hiki tunawakosoa kosoa wazazi wetu kiasi kwamba wanapoteza Mamlaka walizo nazo juu yetu.Fikiria leo Una Mtoto Kila unachomwambia anakuambia wewe hujui ,kinafanywa hivi,Utajisikiaje ?
Iwapo mzazi amepoteza Mamlaka Juu yako jiulize mara mbili mbili kipi kinafwata kwenye maisha yako. Haijalishi unaishi wapi na unafanya nini Mzazi ni Mzazi hakikisha unaitii Mamlaka husika kama Unavyotii Bosi wako Ofisini.
Pamoja na Ujuzi wa Mambo kadha wa Kadha ambayo tunayo huwezi kufika ofisini na kujiamulia kukosoa kosoa utawala kadri unavyojisikia sababu unajua kuliko wao.Mamlaka unapotoa mlango wa kushauri ndipo Unashauri.Fikiri Mungu angekua anasima Mbele ya Wazazi wako ,una muona uso kwa uso Je ungekuwa unamshushua kama unavyowashushua wazazi wako leo? Je Ungekuwa unamrekebisha rekebisha kama Unavyofanya leo ?

Iwapo umeshawahi kufanya hiki kitu Rudi kwa Wazazi wako kaombe Msamaha na kinachofwata watii na ufwate wanachokuambia na haijalishi kina maumivu kiasi gani.Utii ni Bora kuliko Sadaka na Zawadi unazowapelekea kila Krismasi na Pasaka.


(IV) Je umewahi kuwalaumu/Unawalaumu kwa Maisha yako ya Sasa?

Moja ya Kosa ambalo tunafanya kizazi hiki ni kuwalaumu wazazi wetu kwa sababu ya maisha yetu ya Sasa.Kiwango walichokufikisha ndio uwezo wao ulipofikia wa kiakili,kifedha n.k.Kuna watu wengine tumewalaumu wazazi kwa sababu tulidhalilishwa sehemu na baadae kupelekea kuathirika kisaikolojia.Je Angekuwa ni Mungu angesimama mbele yako Ungemlaumu kwa maisha yako ya sasa kwamba amefanya makosa hivi leo ulivyo? Je toka uanze kulaumu lawaza zako zimebadilisha maisha yako binafsi? Je makosa yako yanayokea kazini kwako Una mlaumu Bosi wako kwamba amesababisha?

Kulaumu laumu ni ishara kwamba hauna shukrani,Je ni wangapi wamefikia hatua ulioyofikia leo?Je ni gharama ngapi wametumia kukulea?Je unaweza kuwalipa kwa kila hatua ya malezi uliyopitia,tangu ukiwa tumboni mwa Mama? Lawama ni ishara ya kwamba hauridhiki na walivyokulea kwa Maana nyingine hauna shukrani juu ya kile walishofanya kwenye maisha yako.

”Lawama ni ishara moja wapo ya kutokuwa na heshima kabisa”.

Je huwa kila siku asubuhi ukiamka unamlaumu Mungu kwanini amekuamsha aua hawa kwa sababu hawasemi wanaumia ndani kwa ndani?

Iwapo ulifanya hili tukio nenda kwa Wazazi Kawaombe Msamaha haraka ili siku zako ziwe nyingi na uishi kwa mafanikio.Ni Bora utekeleze maagizo ya Mungu kwa sehemu yako.Hiyo sehemu nyingine kwamba walifanya makosa mwachie Mungu sio kazi yako kuwahukumu.

(V) Je Unatumia Muda gani Kuwasiliana Nao?


“Kitu chochote ambacho kina uwezo wa kuchukua saa 1 katika saa 24 kitu hicho kina thamani kubwa kwako”

.Kitu chochote unachofanya kwa siku kwa Muda wa saa 1 kila siku kwa Muda wa Siku 21,Kitu hicho kinakuwa sehemu ya tabia yako na ni moja ya vipaumbele vya maisha yako maana yake hauwezi kuishi bila hicho kwenye maisha yako.Iwapo Unatumia saa moja kila siku kwenye simu,facebook ,twitter n.k kila siku maana ina thamani kwenye maisha yako na hauwezi kuishi bila hicho.

Kuna tofauti kubwa kati ya kuwasiliana na Mtu na Kumpa taarifa Mtu.Ukitaka kujua aina ya heshima ulio nayo kwa mtu jiulize unampaga taarifa au unawasiliana naye?Kitu chochote kinachotumia muda mwingi kwa siku kwenye maisha yako maana yake unakeheshimu na kina thamani kubwa kwenye maisha yako na hauwezi kuishi bilai hiko.

Jiulize kwamba wazazi wako unawasiliana nao aua huwaga unawapaga taarifa kwa siku na unatumia muda gani kuwasiliana nao kwa siku.Kila siku sisi Wakristo tuna ratiba za kusoma neno na kuomba sababu tunamuheshimu Mungu kwenye kila jambo.Hakikisha unaongeza muda wa kuwasiliana na wazazi wako badala ya kuwapa taarifa ya kila siku za maisha yako.Heshima hujengwa katika muda.


(VI) Je umewahi kuwapa/Unawapa zawadi?


Kuna wakati niluwa na rafiki yangu alikuwa kwenye mahusiano lalamiko lake kubwa ilkuwa Mchumba wake anadai kwamba Yeye apewe zawadi kubwa kuliko Wazazi wa Huyo rafiki yangu.
Asije akakudanganya mtu Zawadi inaongea kuliko maneno matupu ,Zawadi ina nguvu sana ,Zawadi inaonyesha uthamani wa mpewaji.Wazazi ni sehemu ya mafanikio ulio nayo,Wazazi ni sehemu ya ubora ulio nao leo.

Hakuna mtu ambao wamewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye maisha yako kuliko wazazi wako.Je umeshawahi kuwaheshimu kwa kuwapa zawadi? Je Iwapo unawapaga zawadi ina thamani gani? Jifunze kuwapa wazazi wako kilicho bora..Tunapoenda Kanisani kutoa sadaka tunaenda na sadaka nzuri ni ishara ya kwamba tunamuheshi Mungu kwa kile ambacho amefanya maisha kwenye maisha yetu.Je unawezaje kumeheshimu usiyemuona na usimuheshimu unayemuona? Hii ni aina ya kosa ambalo linapelekea uangamivu wa maisha yako. Mbona girlfriend/boyfriend wako unamnunulia gauni/shati boutique lakini wazazi wako una wapelekea nguo za Mtumbani? Wazazi watapokea kwa Shukrani kwa zawadi uliyowapelekea lakini wewe unajua moyoni kile ulichofanya ni sahihi?

“Zawadi inaonyesha thamani na heshima ya Yule Unayompelekea”

Iwapo unataka kuishi miaka mingi yenye Baraka na Mafaanikio hakikisha uboresha aina zawadi unayopeleka na iwapo haujawahi peleka jifunze sasa.

(VII) Je wewe ni Mfano wa Kuigwa?


Moja ya Swali la kujiuliza iwapo una waheshimu wazazi wako “Je wewe ni mfano wa kuigwa”.Wazazi wako wamewekeza miaka Mingi ya malezi na rasilimali nyingi bila wao kutarajia iwapo utawarejeshea kwa kiasi gani kwa sababu wewe ni ulikuwa sehemu ya jukumu lao kukulea kwenye taratibu walizoweza kukulea. Hakuna mzazi anayependa kusikia mtoto wao anafanya hiki na kile ambacho kinapingana na taratibu zao walizokulea ,Haijalishi wao walikosea mara ngapi lakini wewe unapaswa kufwata maelekezo yao ya namna ya kuishi.

Tunafwata maelekezo ya Mungu ya namna ya kuishi kama Ishara ya kwamba tuna muheshimu na kumthamini.Kutofwata maelekezo yake ni ishara kwamba hatumueshimu.

Jiulize ni Mara ngapi wazazi wako wamelia kwa tabia zako mbaya na kadha wa kadha.Ni Mara ngapi unajua kabisa moyoni mwako unayofanya ni kinyume na maelekezo walioyukupa haijalishi wanaona au hawaoni,Kutowaheshimu wazazi wako kwa maelekezo yao ni Ishara ya kwamba Haumeshimu Mungu aliyekuweka kwenye mikono ya malezi yao.

Je wadogo wako wakiletwa waishi na wewe ,Je ni mfano wa kuigwa?Au ndio unasubiri walale ufanye yako? Hili swali ni Binafsi sana.Iwapo unajua wewe si mfano wa kuigwa Jirekebishe uli siku zako za kuishi ziongezeke tena ziwe na faida.

“Kutokutii Maelekezo ya Wazazi waliokupa Wakati wa Malezi ni Ishara ya Kutowaheshimu, Kutowaheshimu wazazi ni kutomuheshimu Mungu”

HITIMISHO

Kuna Maswali Kadha wa Kadha unaweza uka nayo pia unaweza kujiongezea ya kwako pia.Baada ya Kusoma makala hii jiulize “Una waheshimu wazazi wako kwa kiasi gani?” Baada ya kumaliza kujiuliza fanyia kazi,Itakuwa ni kazi bure usoma na ujiulize maswali alafu usifanyie kazi maana unaweza ukakuta unazunguka pale pale kila siku.

Kwa wale ambao ni wazazi Hakikisha Unajenga Utaratibu wa Kuwafundisha watoto kuwaheshimu ninyi ndipo wataweza kumuheshimu Mungu.Haiwezekani Wakamuheshimu wasiyemuona huku wasimheshimu wanayemwona kila siku.Wazazi ili watoto wenu wawe na maisha marefu nay a Baraka wafundisheni kuwaheshimu kwa bidii haijalishi ni ngumu kiasi gani hii itaokoa nafsi zao na laana ya Mungu.

“Mzazi anayeruhusu Watoto Kumtomuheshimu Mzazi Mwingine Anawaangamiza Watoto Wake Mwenyewe”

Mwisho “Maisha yamejengwa kwenye Mfumo wa Heshima “ndio Maana tunanaishi fikiria tusingekuwa tunaheshimiana nini kingetokea?

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.