MORAVIAN DAR ES SALAAM WAPATA JIMBO KAMILI LA MASHARIKI

Hapo jana katika viwanja vya kanisa Moravian, Mbagala chamazi jijini Dar es salaam kulifanyika tukio kubwa la kuukaribisha mwaka mpya pamoja na kupokea rasmi jimbo la Mashariki la kanisa hilo ambalo makao makuu yake yatakuwa hapo Chamazi. Awali jimbo hilo lilikuwa likifahamika kama jimbo la misheni mashariki na Zanzibar ambapo mgogoro mrefu ndani ya kanisa hilo na jimbo ambao hata hivyo haijulikani kama umemalizwa au bado upo.

Mgogoro ulifanya kanisa hilo kuingia kwenye matatizo mazito ikiwemo baadhi ya waumini wa kanisa kupigana na watumishi wao ama kufikishana polisi na wengine kufikia kufanya ibada nje ya majengo yao ya kanisa na kufanya kuwepo na mgawanyiko baina ya sharika za kanisa hilo hususani jijini Dar es salaam na Morogoro. Jimbo jipya kamili lilitangazwa na mwenyekiti wake mchungaji Samuel Mwaiseje na ibada hiyo kuhudhuriwa na waumini,waimbaji na wageni mbalimbali wa kanisa hilo.

Mwenyekiti wa jimbo la mashariki mchungaji Samuel Mwaiseje
Mchungaji Mwaiseje akizungumza na waumini pamoja na wageni waliofika katika tukio hilo 
Wachungaji wa jimbo la Mashariki wakiwa ibadani
Wachungaji wakishikwa mikono
Baadhi ya waumini wakiwa ibadani
Baadhi ya waumini katika picha
Amani kwaya Mabibo wakimsifu Mungu
Amani kwaya wakiimba
Baadhi ya viongozi na watumishi wa kanisa hilo
Viongozi wakipewa mkono na mtumishi
Kwaya ya vijana wakati wakimtukuza Mungu
Kwaya kuu ya jimbo na Amani kwa mbali wakiwa wamesimama wakati wa ibada hiyo 
Waimbaji na baadhi ya waumini waliokuwepo ibadani hapo jana Chamazi
Amani Choir kutoka Mabibo Moravian wakiwa wamesimama
Waimbaji wa kwaya kuu ya jimbo wakiwa ibadani hapo©Asulwisye Mwalupani


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.