MSAADA WAKO KWA MAMA HUYU UNAHITAJIKA

Na Sia Lyimo.

Bi Lucia (kulia) akiwa na watoto wake wawili pamoja na wajukuu zake kwenye chumba ambacho amepata hifadhi
Historia ya Lucia Kasembe Michenga ni ndefu, ni mama mjane mwenye watoto watatu na wajukuu watatu. Ni mwenyeji wa Masasi, Mtwara. Ambaye alikuja Dar es Salaam kwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya jicho lakini kutokana na hali yake kuwa mbaya ilimbidi abaki Dar es Salaam pamoja na familia yake.

Kufuatia hilo, kanisa la International Pentecostal Holliness (Benaco Salasala) lilimpokea mwanzoni mwa mwezi Disemba kwa ajili ya maombezi lakini kutokana na hali ngumu ya maisha aliyonayo yeye na wanae wanaomuhudumia, kanisa limekuwa likiwasaidia kwa chakula, madawa na matumizi mengine."

Nyumba anayoishi Bi Lucia na binti zake.
Maisha yaliendelea na akapatikana msamaria mwema aliyempangishia chumba maeneo ya Tegeta Kwa Ndevu ambapo amekaa kuanzia mwezi wa tisa 2014. Kutokana na hali yao ya kipato kuwa duni, wameshindwa hata kupata chakula wakati mwingine.

Nyumba inalipwa 25,000 kwa mwezi, ila mpango uliopo sasa ni kumtafutia nyumba sehemu nyingine kwani mazingira sio salama kwake kulingana na hali aliyonayo.

Mchungaji Shadrack akiwa na familia ya Bi Lucia.
"Sisi kama kanisa tumeona kwamba upendo wa Mungu unaanzia kwa kupendana sisi wanadamu kwanza. Hivyo tumeamua kuwasaidia familia hii kiroho na kimwili. Tunaomba watu wote wenye mapenzi mema kuungana nasi katika kuitegemeza familia hii." Anaeleza Mchungaji Shadrack Msogoya.

Kwa msaada wowote, unaweza kufikishwa kupitia namba 0755237785, ambayo ni namba ya Mchungaji Shadrack.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.