MWIMBAJI WA WIMBO 'OMBEA ADUI YAKO' APATA AJALI MBAYA NCHINI KENYA


Mwimbaji nyota wa wimbo 'Ombea Adui Yako' Peace Mulu kutoka nchini Kenya amepata ajali mbaya ya gari siku ya jumatatu kwenye barabara ya Kangundo nchini kwao Kenya na kuvunjika mfupa wa paja la mguu wake wa kuume ambapo anatagemewa kufanyiwa upasuaji siku ya leo katika hospitali ya kimataifa ya Kenyatta jijini Nairobi.

Mwimbaji huyo alikuwa pamoja na wenzake walikodi magari ya abiria almaarufu kama matatu wakitokea kwenye shughuli ya kurekodi video na kukutana na ajali hiyo ambayo iliwaacha wamiliki wa matatu watatu wakijeruhiwa huku wenzake wawili ambao pia walijeruhiwa katika ajali hiyo walipatiwa matibabu na kuruhusiwa huku yeye akilazwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi hususani upasuaji unaofanyika hii leo.
Miguu ya Peace hospitalini.

Kutokana na ajali hiyo waimbaji na wanamuziki nchini Kenya wanakutana hii leo katika hoteli ya Accra kwaajili ya kuchangishana pesa ili kusaidia kulipa bili ya matibabu ya mwimbaji mwenzao. Kwa mujibu wa bwana Mutisya Maweu anayejihusisha na mambo ya hati miliki za waimbaji nchini Kenya ambaye pia ndio anahusika katika kuwakusanya waimbaji nchini Kenya kufanya kitu kwaajili ya Peace amesema mwimbaji huyo yupo katika hali nzuri ingawa yupo katika maumivu mazito

"alitakiwa kufanyiwa upasuaji siku ya jumatano ila kwakuwa tulikuwa tunafanya mpango wa kuhamishiwa katika hospitali binafsi hivyo upasuaji ukasogezwa mbele" alikaririrwa Mutisya akiongea na nairobinews.com. Peace Mulu amekuwa kwenye tasnia ya muziki wa injili kwa zaidi ya miaka 14 sasa akiimba mziki ya injili pamoja na siasa akifadhiliwa na wanasiasa pia amewahi kupendekezwa  pamoja na kushinda kwenye kinyang'anyiro cha kugombea tuzo za Groove Awards kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka kutoka mashariki ya Kenya. Nchini Tanzania amefahamika kupitia wimbo wa 'Ombea Adui Yako aishi siku nyingi'.

Peace Mulu akiwa kwenye maumivu mazito hospitalini. picha kwa hisani ya Abednego Hango


Mkumbuke kwenye maombi mtumishi huyu wa Mungu. 

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.