NAMNA YA KUFIKIA MALENGO KWA USAHIHI NA UBORA ZAIDI

Na Faraja Naftal Mndeme

©John Boyens Blog
1. Hakikisha unakuwa na Mpango kazi wa siku.
Wakati mwingine Watanzania wengi tumefikiri tuna muda mwingi na hata jambo tusipolitekeleza leo kesho ipo tu tutafanya lakini kiukweli nani ajuaye ya kesho? Hakikisha utendaji wako wa kila siku haupotezi muda pasipo sababu ya msingi. Linalowezekana kufanywa leo kwani lisubiri kesho?

2. Hakikisha Unaongeza Ufanisi wako wa Kila Siku.
Muda mwingine tumefiria malengo makubwa hutokea mara moja lakini kiukweli matokeo makubwa tunayoyaona kwa watu ni mkusanyiko wa kazi ndogo ndogo za kila siku ambazo zilifanywa kwa ufanisi wa hali ya juu bila kuupuzia udogo wa jambo husika.

3. Ongeza ufahamu kila siku kuelekea kutimiza malengo yako.
Mara nyingi tumetumia muda mwingi kufikira namna ya kufikia malengo lakini tumesahau kujifunza mambo kadha wa kadha wakati tunaelekea kufikia mafanikio ya malengo yetu. Muda mwingine unaweza usifanikiwe kufikia malengo uliyojipangia kwa asilimia 100, lakini hata usipofikia umejifunza kitu gani? Mafanikio unayofikia yakuongeze ufahamu pia ya kufanye kuwa mtu bora zaidi.

4. Punguza makosa madogo madogo kila siku.
Ufanisi mkubwa unaouona kwa watu leo ni mkusanyiko wa ufanisi mdogo mdogo na utendaji wa kila siku. Hakuna makosa ambayo yanatokeaga ili mradi kutokea. Makosa madogo madogo ya kila siku ndio yanayoweza pelekea anguko lako kubwa kwa wakati ujao. Hakikisha makosa ambayo yanafanywa kila siku yanapunguzwa kadri iwezekanavyo.

5. Tathmini ya Kila Siku.
Jijengee tabia ya kuwa na tathmini ndogo ndogo za kila siku juu ya malengo yako. Tathmini za kila siku zitakusaidia kupunguza makosa na kukusaidia kuwa na mtazamo bora zaidi wa kuweza kufikia malengo ambayo umeyatarajia kwa kipindi husika. Hakikisha unafanya hivyo hili kuweza kufikia malengo yako kwa upesi na kwa ufanisi mkubwa zaidi. Pia tathmini za kila siku zitakusaidia kufahamu iwapo unasonga mbele au hapana.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y'All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.