NINAWEZA KUIMBA: HATUA YA UCHAMBUZI MEZANI

Zoezi la kusaka vipaji vya uimbaji kwa ajili ya kumuinulia BWANA Yesu utukufu, Ninaweza Kuimba limefikia hatua ya uchambuzi, ambapo sauti za washiriki zimewekwa mezani kuona sauti ya nani inaweza kupelekwa studio, kati ya washiriki zaidi ya hamsini waliojitokeza.

Upokeaji wa sauti za Ninaweza Kuimba ulianza rasmi tarehe 19 Novemba 2014, ambapo baada ya wiki tatu za awali, muda uliongezwa hadi Disemba 24 saa sita usiku.

Kwa tathmini ya awali, imeonekana dhahiri ya kwamba wigo wa ushiriki kwenye mikoa mingine unahitajika, kwani watu kadhaa kutoka nje ya mikoa husika ya Dar es Salaam na Arusha walipiga simu kwa ajili ya kuuliza na hata kutuma jumbe kupitia WhatsApp.

KIFUATACHO
Uhakiki wa sauti utafanywa kwa nyakati mbalimbali ndani ya wiki 2 ili kuthibitisha kwamba aliyetuma ndiye. Vinginevyo kuwa na mshiriki sahihi aliyekidhi vigezo na masharti. Unachotakiwa kufanya ni kuendelea kufuatilia Gospel Kitaa ili taarifa mpya zisikupite kuhusiana na shindano hili ama kwa habari nyinginezo zozote.

Washindi watafahamishwa kupitia hapahapa Gospel Kitaa na pia kupitia Gospel Celebration ya WAPO Radio FM.

GK tayari iko kwenye mjadala na walimu mbalimbali ili kutambua ni sauti gani ikinolewa japo kidogo itafanya vyema zaidi, na hata kujua nyimbo inayoweza kufaa kwa ajili ya washiriki waliojitokeza.

Wadau ambao kwa sasa tunaweza kuwataja ni pamoja na ArakaPro Media, JM Media, pamoja na InHouse Pictures.

2015, kwa pamoja tunavuka na ushindi wa kipekee. Tunakutakia wakati mwema. Na kwa washiriki wote, tunawatakia kila la heri.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.