NYOTA WA JOYOUS CELEBRATION AMTAKIA HERI YA KUZALIWA MTALAKA WAKE, AMTAKIA MAISHA MEMA

Sphumelele Ntokozo Mbambo akiwa na mumewe bwana Sakhile siku ya harusi yao mwaka 2012
Mwimbaji nyota wa kundi la Joyous Celebration mwanadada Sphumelele Mbambo ameamua kuvunja ukimya na kuujulisha umma wa mashabiki, ndugu na marafiki zake kupitia mtandao wa Facebook kwamba ndoa yake ilivunjika katika maelezo ya mwimbaji huyo akimtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa mtalaka wake.

Habari hiyo ya kuhuzunisha na kustusha iliwekwa wazi na mwimbaji huyo anayependa kuimba nyimbo za injili za kitamaduni ama za Zion (Sayuni) kama wanavyoziita wakazi wa nchini humo, kwamba anamtakia heri ya kuzaliwa na maisha yenye mafanikio huko aendako na yeye (Ntokozo) atakuwa nyuma yake kama dada akimuombea ili afanikiwe katika kila jambo atakalokuwa akifanya.

Aidha Sphumelele ambaye jina lake lingine ni Ntokozo amesema ataendelea kumuombea kwa Mungu kwamba ambariki na pia kujifunza kupitia makosa yake na pia kupitia uzoefu wa ndoa yao alioupata atawasaidia na wengine kwakuwa watu hujifunza na makosa na kumalizia kumtakia heri katika maisha yake kwa mumewe huyo ingawa haijaelezwa kama wamepeana talaka.

Sphumelele Ntokozo Mbambo ambaye awali kabla hajaolewa aliwahi kukimbiwa na mwanaume wa kwanza aliyezaa naye mtoto (GK iliwahi kuandika historia yake bonyeza HAPA) alifunga ndoa na bwana Sakhile Thomas Mthembu ama mwite Dj Kiteng kwa jina lake la kazi za muziki mwezi March 2012 kabla mwanaume huyo naye kuamua kumuacha mwimbaji huyo ambaye kwa taarifa aliyotoa kupitia ukurasa wake wa Facebook imepokelewa kwa hisia kali na marafiki zake ambao wengi wamempongeza mwimbaji huyo kwa moyo wake wa ujasiri kuweka mambo yote hadharani kuliko kuacha tetesi kuchukua nafasi.

Sphumelele akiwa na mtoto wake matembezini mapema mwaka jana 


Aidha mashabiki hao wamemtakia baraka za Mungu mwimbaji huyo na kumwambia kwamba Mungu atambariki kwa kitendo alichofanya na kuonyesha kutokuwa na kinyongo naye tena huku wengine wakimtaka mwimbaji huyo kutulia kwakuwa kwa mujibu wa Biblia takatifu bwana Sakhile bado ni mumewe halali huku mwimbaji huyo akijibu kama ni mali yake atakuja ila kama si wake hawezi kumlazimisha.Sphumelele akiwa katika jukwaa la Joyous akimsifu Mungu
Chini ujumbe aliouandika Sphumelele katika ukurasa wake wa Facebook

Namuhla kuZalwa My Ex husband indoda okwakumele ngiguge naye engabona ubuudoda kuye ngokungikhetha kwabaningi wangenza umkakhe uSakhile Thomas Mthembu nakuba singaphelelananga kodwa uyindoda yamadoda uyisibusiso lolusuku lusho ukuthi kuningi okuhle okusamele akwenze emhlabeni ngimufisala impumelelo nenjabulo yaphakade ame aqine isibindi kuningi esike zizitshele ukuthi okwethu kanti cha uJehova usahlela yebo Wangala and ikhula ngamaphutha kodwa lokho akumenzi isilwane indoda ikhula ngokuwa im praying for you ukuthi uJehova akubusise ngakho konke okufisayo akupholise amanxeba asenhlizweni yakho ube indoda ezokwakha amanye amadoda kusasa from your experiences hlala wazi kuningi okuhle ngawe manje usufana noBhuti wami sekwadlula nokukhala ngikufisela uThole umfazi ozokuthanda akuhloniphe nibe umndeni lonyaka ungowesibusiso wena uNgoka Jehova Happy birthday Dj Kiteng my Ex Hubby enjoy your day


Wakati huohuo kuna tetesi ambazo si nzuri kwa ndoa ya mwimbaji mwingine wa Joyous ambaye mwaka jana mwezi june alitimiza mwaka mmoja wa ndoa yake kwamba ameachana na mumewe na kuamua kurudi kwao CapeTown kujiunga na familia yake toka julai mwaka jana. Wasiwasi kuwepo kuvunjika kwa ndoa hiyo ni kutokana na mwimbaji huyo aliyejiunga mwaka mmoja na Sphumelele ndani ya Joyous wakitokea katika shindano la I want to sing gospel ni vitendo vya yeye na mumewe kutoonyesha kama kuna ndoa kati yao kwa kuweka picha mbalimbali wakiwa na watu wengine ama wakifurahia maisha sehemu mbalimbali bila kuwa pamoja.

Wanandoa hao kuna wakati huyu akionyesha yupo nyumbani anaangalia sinema mwingine mda huo ataposti picha yupo kwenye sherehe na marafiki zake hali ambayo imefikia mashabiki kumuuliza mumewe kupitia anuani yake ya Instagram kwamba nini kinaendelea kati yake na mkewe ama wameachana? mpaka leo hakuna jibu mke yupo kwao CapeTown mume yupo kwake Johannesburg. Hata hivyo kwenye ukurasa wake wa Facebook mwanamke bado hajatoa jina la mumewe huku upande wa mumewe ambaye pia anafanya kazi za mtandao ndani ya kundi hilo akiwa hajaweka taarifa yake ya mahusiano.

Joyous Celebration 15, ni waimbaji watatu tu katika picha hii bado wapo na kundi hilo


2014 haukuwa mwaka mzuri kwa tasnia ya muziki wa injili sehemu nyingi. Mdau wa GK kumbuka kuchukua hatua ya kuwaombea watumishi wa Mungu, waimbaji na wengineo ili Mungu awasimamishe na kuwashindia majaribu wanayopitia na kikubwa zaidi tuache tabia ya kuhukumu, ukweli wa mambo wanaujua wanandoa wenyewe. Jukumu letu kuwaombea na si kufurahi tusikiapo taarifa mbaya kutoka kwao. BarikiwaShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.