PATA UPAKO WA KWENDA SAWA 2015 NDANI YA CHAGUO LA GK

Mchungaji Mthunzi Namba
Heri ya mwaka mpya msomaji wa GK, kumbuka ni neema tu ya Mungu kwamba tumeweza kuuona mwaka mpya wa 2015, si vingine vyovyote vile kwamba tubauwezo mkubwa sana kuliko wengine waliotangulia ila ni 'NEEMA' tu ya Mungu imetuwezesha kutupa nafasi nyingine ya kuishi kwa mwaka huu. Basi jumapili ya leo, tumekuchagulia wimbo kutoka kwa mmoja wa waanzilishi wa kundi maarufu la muziki wa injili Afrika Joyous Celebration aitwaye mchungaji Mthunzi Namba.

Kutoka kwake tumekuchagulia wimbo 'Mercy' kutoka katika album yake binafsi aliyorekodi huko Durban Afrika Kusini mwaka 2009, akiwa amewashirikisha waimbaji wa Joyous enzi hizo wakingali kundini. Tunatumaini utabarikiwa na wimbo huu ambao ndio uliobeba album hii ukiwa unazungumzia zaidi habari ya neema ya Mungu inavyotuwezesha kuanza upya kwa maisha yetu haijalishi ni mambo gani tumeyatenda kabla ama sisi ni watu wanamna gani ila rehema zake na neema zinatusimamisha kwa upya. BarikiwaShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.