PENGO SI MWANYA, NA MWANYA SI PENGO

Na Faraja Naftal Mndeme
GK Contributor

©Kensington Clinic
Ni rahisi mtu tajiri akifilisika kurudi kuwa tajiri, kuliko mtu maskini kuwa tajiri. Matumizi ya rasilimali ambazo tumepewa hapa duniani ni kitu muhimu sana. Kuna aina nyingi za rasilimali kwenye kufiki hatma ya maendeleo ambayo tunayataka. Mungu alipotuweka hapa duniani alitupa uwezo na akili tuweze kushirikiana pamoja naye katika uumbaji wa nchi hii ndio maana alipotuumba alituweka rasilimali ghafi (raw materials) badala ya kututengenezea kila kitu. Mungu hakushindwa kutengeneza maghorofa au vitu vingine tunavyovihitaji kisha akauweka tufurahie maisha yetu lakini badala yake aliona tutaboreka hapa kwenye sayari hii. Fikiria tangu unazaliwa mpaka una kufa yaani mwaka mmoja hadi sabini kazi yako iwe kula kulala hakuna kingine cha kufanya ungejisikiaje?

Hakuna mtu ambaye aliumbwa na mungu hapa duniani kwa bahati mbaya, tulichotofautiana ni mazingira tuu ya utungwaji mimba na eneo la kuzaliwa lakini mwisho wa siku wote tuko hapa kwenye sayari hii. Mfano, samaki aliyevuliwa kwa nyavu na mtego wote wamevuliwa na wote tunawakuta sokoni, yaani mwisho wa siku tunawakuta kwenye tenga la mvuvi. Mungu hakoseagi kuumba wala kupanga. Kila alichokiumba ni bora na tena kina uwezo kamili na kinaweza kuishi kulingana na mipango na mazingira aliyokitengenezea. Kusema umeumbwa kwa bahati mbaya ni kumtukana aliyekuumba.

Mungu alipomuumba mwanadamu aliweka rasilimali ambazo zitamtosheleza mpaka mwisho wa uhai wake. Mpaka sasa dunia ina takribani watu karibia bilioni 8, lakini hakuna siku umesikia dunia imejaa mpaka watu wakakosa pa kukaa. Kama haiwezi kujaa basi hata rasimali za kutufanya tuishi zipo na zinatutosha bila hata mmoja kupunjika, akili yako ionavyo ndivyo utakavyokuwa. Mungu Ameweka namna ya ajabu ambayo inatutofautisha sisi na viumbe wengine. Viumbe wengine hufikiri kula, kalala kuzaliana na kufa lakini binadamu tumekuwa na uwezo wa kufikiria zaidi ya hapo. Je tunafanyanye kwenda zaidi ya hapo? Ukiona wewe unafikiria kula, kulala, kuzaliana na kufaa hauna tofauti na mnyama mwingine yeyote bali unapofikiria zaidi ya hapo ndipo tofauti yako na wanyama wengine inaonekana.

Wakati tukiwa tumepewa uwezo wa kuzitumia rasilimali zlizopo kwenye sayari yetu na hatuzitumii ni kama kujaribu kufanya pengo lionekane kama mwanya. Unapojilazimisha kuishi maisha yasiyo yako ni sawa na kujaribu kulifanya pengo la mdomoni lionekane kuwa mwanya ili hali pengo ni jino limeng'olewa na mwanya ni nafasi ambayo ipo yenyewe imetokanama na uasili wa maumbile ya mdomo. Mungu alijua kabisa utahitaji kitu fulani wakati unaishi hapa kwenye sayari ndio maana akakuwekea na mazingira ya kukipata.Akili Ulio nayo ndio muujiza wako ndio utajiri wako. Tutumie fursa ambazo zipo kuweza kujiletea maendeleo tuache kuleta vingizio visivyo na maana.

Wakati unaumbwa hakuna mtu ambaye alipewa wajibu wa kukufanya wewe uendelee mbele bali wewe ndio unapaswa kujiendeleza. Hakuna sehemu yoyote kwenye kitabu chochote cha dini ambacho kimeandikwa ukishazaliwa utaikuta serikali na serikali itakufanya ufikie malengo yako ya kimaisha kwa kuitegemea. Je iwapo kusingekuwa na serikali ungemlaumu nani? Tufanye kwanza kwa sehemu yetu ndipo tuwatupie lawama wengine. Tusianze kulaumu ili hali hata hatua moja haujapiga.

Ukiamua kufikia malengo fulani ya kimaisha utafikia tu ku-amua kufikia malengo haya inategemea kiasi gani umejipanga kufikia malengo yako.Fursa Zipo na zitaendelea kuwepo hazitaisha siku zote za maisha yetu.Tulizikuta Na tutaziacha kinachopaswa ni wewe binafsi kusimama na kutetea hatma yako binafsi na kwa kufanya maamuzi sahihi.Maamuzi Ndio yanayotofautisha watu wote.

Ubongo wa mwanadamu ni mithili ya hardaware ya computer na taarifa zinazoingia kwenye ubongo ni mithili ya operating system inayokuwa-installed kwenye ubongo.Unapoona Computer haifanyi kazi vizuri nenda kaangalie hiyo operating system iliyokuwa installed ni sahihi.. Unaweza ukakuta computer yako inahitaji windows 94 wewe unailazimisha window 8 na ubuntu kitu ambacho hakipo. Ukitaka matokea mazuri ya computer ifanye kazi tafuta recommended operating system ndio u-install kwenye computer yako hali kadhalika kwenye ubongo ndivyo kulivyo; tafuta proper information ndio uweke kwenye ubongo wako ili kuweza kupata matokeo thabiti na sahihi ya kile unachokihitaji.

Kwenye uhalisia wa fikra hakuna mtu ambaye hana ajira ila wapo watu ambao hawataki kuajiriwa. Tumezoeshwa formal way ya kuajiriwa yaani kwenda ofisini na kurudi. Unaweza kuamua kufanya kitu kingine na ukafikia malengo bila tatizo tusijaribu kutafuta visingizio visivyo na maana kwa kuwabebesha wengine mizigo yetu wenyewe. Kutokuendelea kwako ni uamuzi wako mwenyewe...


E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God bless y’all

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.