SOMO: KWANINI HUKUOGOPA? - MCHUNGAJI GWAJIMA

Mchungaji Josephat Gwajima
2SAMWELI 1:1-
Daudi alikuwa mwenye miaka 16 alimuua goriat na Mfalme Sauli akapata hisia kwamba huyu kijana kwa nguvu zake anaweza kuwa Mfalme ndipo Daudi akakimbilia kwa elimeleki kujificha huko na kuhani alipopata habari Daudi amesaidiwa naye akamuua Elimeleki kwasababu alimpa Daudi chakula. Daudi akakimbizwa porini akakaa huko miaka mingi. Sauli akaamua kupigana na wafilisti akaachana na Daudi.

Wakati Daudi yuko jangwani na siku moja akamuona kijana anakuja akatoa taarifa za vitani kumwambia Daudi kwamba watu wamekimbia vitani tena watu wengi wameanguka wamekufa na hata sauli na Yonathani mwanaye amekufa na Daudi akamuuliza “umejuaje Sauli amekufa”? ndipo kijana yule akamuelezea kwamba Mfalme alipigwa mshale ameanguka chini na akaniiambia nimmalizie ili asije kushikwa akiwa hai kwasababu alijua hakika hata pona baada ya kuanguka chini na mshale na ndipo akamuua. Daudi aliposikia hayo akararua mavazi yake akayatupa chini pamoja na mashujaa wake wakaacha kula mpaka jioni wakiumwombolezea Sauli masihi wa Bwana.

Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya; (kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema, Wana wa Yuda na wafundishwe haya, Walio fahari yako, Ee Israeli Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa; Jinsi mashujaa walivyoanguka! Msiyahubiri mambo haya katika Gathi, Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni; Wasije wakashangilia binti za Wafilisti, Binti za wasiotahiriwa wakasimanga. Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta. Kutoka kwa damu yao waliouawa, Kutoka kwa shahamu yao mashujaa, Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, Wala upanga wa Sauli haukurudi bure. Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza Maishani wala mautini hawakutengwa; Walikuwa wepesi kuliko tai, Walikuwa hodari kuliko simba. Enyi binti za Israeli, mlilieni Huyo Sauli, ambaye aliwavika Mavazi mekundu kwa anasa, Akazipamba nguo zenu dhahabu. Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita! Ee Yonathani, wewe umeuawa Juu ya mahali pako palipoinuka Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake. Jinsi mashujaa walivyoanguka, Na silaha za vita zilivyoangamia!

Baada ya kuwa amemaliza kumlilia akaamka jioni akamwendea yule kijana akamwambia

1SAMWELI1:14-16
Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA? Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hata akafa. Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa Bwana.

Kwa desturi wayahudi mtu awezi kuitwa masihi hadi amwagiwe mafuta na ndiomaana walimkataa Yesu kwasababu alijiita Kristo “masihi wa Bwana” uungu wa Mungu juu ya mwadamu mwanadamu anakuwa ana vipande viwili uwanadamu wake na uungu ulioko ndani yake, kwenye agano la kale mtu alitakiwa amwagiwe mafuta ndipo aitwe “masihi wa Bwana” na kwenye agano jipya mtu mpaka ajazwe Roho mtakatifu na Yesu alipobatizwa lilishuka wingu zito kutoka juu na sauti ikasikika na kitendo hicho ni kumwagiwa roho mtakatifu kwa namna ya rohoni.

Huyu kijana alipo muua sauli alienda kwa Daudi akiwa na furaha kwamba alimuulia adui wake lakini Daudi akamuua kwasababu alimuua masihi wa Bwana. Sauli alikuwa amerudi nyuma lakini Mungu alimuona kama masihi wake na Daudi naye alilifahamu hilo. Sauli hakuuwawa na yule kijana bali alitaka sifa ili Daudi ampongeze na asheherekee lakini alimkuta amekwisha kufa.

Zaburi105:15
Kama kinywa chako kinawasema vibaya masihi wa Bwana utapata laana sio vizuri.

Dada yake na Musa alikuwa anaitwa Miriam alishughulika kwenye kumficha Musa.

Hasabu12:1-
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa? Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake. Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana. Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena. Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.

“Watu hawawi watumishi wa Mungu kwasababu wametaka bali ni kwasababu Mungu amewachagua wawe” wakati mwingine safari ya kiroho ya mtu inaweza kukwama kwasababu ya kuwasema watumishi wa Bwana.

Hesabu16:1-35
Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni; nao, pamoja na watu kadha wa kadha wa wana wa Israeli, watu mia mbili na hamsini, Wakuu wa mkutano, waliokuwa wateule wa mkutano, watu wenye sifa, wakainuka mbele ya Musa; Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Jitengeni ninyi mkaondoke kati ya mkutano huu, ili nipate kuwaangamiza mara moja. Nao wakapomoka kifudifudi, wakasema, Ee Mungu, Mungu wa roho za wenye mwili wote, je! Mtu mmoja atafanya dhambi, nawe utaukasirikia mkutano wote? Bwana akasema na Musa, na kumwambia, Nena na mkutano, na kuwaambia, Ondokeni ninyi hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani, na Abiramu. Basi Musa akainuka na kuwaendea Dathani na Abiramu; na wazee wa Israeli wakaandamana naye. Akasema na mkutano, na kuwaambia, Nawasihi, ondokeni penye hema za hawa watu waovu, wala msiguse kitu chao cho chote, msiangamizwe katika dhambi zao zote. Basi wakaondoka hapo karibu na maskani ya Kora, na Dathani na Abiramu, pande zote; nao kina Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama mlangoni mwa hema zao, pamoja na wake zao, na wana wao na watoto wao wadogo. Musa akasema, Kwa jambo hili mtajua ya kwamba Bwana amenituma, ili nifanye kazi hizi zote; kwa kuwa mimi sikuzifanya kwa akili zangu mwenyewe. Kama watu hawa wakifa kifo cha sikuzote, kama watu wote wafavyo, au kama wakipatilizwa kwa mapatilizo ya watu wote; hapo basi Bwana hakunituma mimi. Lakini Bwana akiumba kitu kipya, na hiyo nchi ikifunua kinywa chake na kuwameza, pamoja na wote walio nao, nao washukia shimoni wali hai; ndipo mtatambua ya kwamba watu hawa wamemdharau Bwana Basi ilikuwa, hapo alipokwisha kusema maneno haya yote, nchi iliyokuwa chini yao ikapasuka; nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Basi wao, na wote waliokuwa nao, wakashukia shimoni wali hai; nayo nchi ikawafunika wakaangamia kutoka mle mkutanoni. Nao Israeli wote waliokuwa kando-kando yao wakakimbia kwa ajili ya kilio chao; kwa kuwa walisema, Nchi isije kutumeza na sisi. Kisha moto ukatoka kwa Bwana, ukawateketeza hao watu mia mbili hamsini waliofukiza uvumba.

1SAMWELI24:1-6
Ikawa, Sauli aliporudi baada ya kuwafuatia Wafilisti, aliambiwa ya kwamba, Daudi yuko katika nyika ya Engedi. Ndipo Sauli akatwaa watu elfu waliochaguliwa katika Israeli wote, akaenda kumtafuta Daudi na watu wake juu ya majabali ya mbuzi-mwitu. Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, na huko kulikuwa na pango; Sauli akaingia ndani ili kuifunika miguu. Na Daudi na watu wake walikuwa wakikaa mle pangoni ndani sana. Nao watu wa Daudi wakamwambia, Tazama, hii ndiyo siku ile aliyokuambia Bwana, Angalia, nitamtia adui yako mikononi mwako, nawe utamtenda yo yote utakayoona kuwa mema. Basi Daudi akainuka, akaukata upindo wa vazi lake Sauli kwa siri. Lakini halafu, moyo wake Daudi ukamchoma, kwa sababu amekata upindo wa vazi lake Sauli. Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA,neon hili,kuunyosha mkono wangu juu yake,kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

10 Tazama, leo hivi macho yako yameona jinsi Bwana alivyokutia mikononi mwangu pangoni, na watu wengine wakaniambia nikuue; lakini nikakuacha; nikasema, Sitaki kuunyosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Daudi alikuwa anakimbizwa na sauli amelala na walinzi wake wamelala, wale mashujaa wa Daudi wakamwambia hii ndio siku ile aliyoisema Bwana atamweka adui yake mikononi mwako lakini Daudi akakataa hilo na alipojaribu kukata kipande cha nguo yake ili baadaye aje amwonyeshe kwamba alimkuta akamwacha bila kumuua lakini alipokikakata moyo wake ukamchoma kwasababu alikata nguo ya masihi wa Bwana.
Ikatokea siku nyingine Daudi akamwona sauli amelala.

1SAMWELI26:
Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi. Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia.

1SAMWELI28:11
Hasha! Nisiunyoshe mkono wangu juu ya masihi
12 Basi Daudi akalitwaa lile fumo, na lile gudulia la maji, kichwani pa Sauli; nao wakaenda zao, wala hapana mtu aliyeliona jambo hili wala kulijua, wala kuamka; maana wote walikuwa wamelala; kwa kuwa usingizi mzito kutoka kwa Bwana umewaangukia.
Daudi alichukua gudulia la maji akaenda kwa mashujaa akawaambia yie mlistahili kufa kwasababu hamkumlinda masihi wa Bwana. Masihi wa Bwana sio lazima awe kanisani kwako anaweza kuwa mtu mahali pengine.

KUTOKA22:28
28 Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako.
Ilikuwa mojawapo ya sheria ya wayahudi agano la kale, Kadiri maisha yanavyoendelea duniani kuna mahali hauwezi kuingia bila Baraka za Mungu
Maombi haya ya leo yanalenga kuondoa dhambi ndani yako kama hukujua kuongea maneno mabaya juu ya mtumishi wa Mungu yeyote inaleta laana kwenye maisha yako hata kama haitokei leo lakini lazima itatokea hata kama ni miaka ijayo awe ni mtumishi wa kanisani kwako au kanisa lingine mdogo au mkubwa leo fahamu ya kuwa ni dhambi kubwa na hakika inaleta laana kwenye maisha yako.

MWEZI WA KWANZA KUTAKUWA NA MFUNGO WA SIKU 30 KAWE TANGANYIKA PAKERS UFUFUO NA UZIMA KWAAJILI YA KUIBOMOA SERIKALI YA KISHETANI NA MAPEPO YANAYOTAWALA SIKU MFANO SIKU YA JUMA TATU NA MAPEPO YANAYOITAWALA MKARIBISHE NA MWEZIO NA MUNGU AKUSAIDIE TUMIA NAFASI HII JAPO NI VIGUMU KUOMBA MWEZI MZIMA LAKINI JARIBU UONE BAADA YA MAOMBI MUNGU ATAKUTENDEA KITU GANI OMBA RUHUSA KAZINI AU LIKIZO ILI UJUMUIKE NA UTIISHE, UMILIKI NA KUTAWALA MWAKA 2015 KWA JINA LA YESU KRISTO AMEN.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.