SOMO: MAOMBI KUAHIRISHA MABAYA KWASABABU YA MAKOSA YETU - MCHUNGAJI GWAJIMA


SIKU YA TATU YA KUOMBA MAOMBI YA KUAHIRISHA YALE MABAYA AMBAYO MUNGU AMEYAPANGA YATUPATE KWASABABU YA MAKOSA YETU 2015
ASKOFU MKUU JOSEPHAT GWAJIMA

Mwaka 2015 utakuwa ni mwak wa kuijaza nchi, kutiisha na kutawala lakini huwezi kuyapata yote hayo bila kusahihisha mahali tulipo kosea.
Daneli9: 2 Bwana akamtia Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika mkono wake, pamoja na baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mungu; naye akavichukua mpaka nchi ya Shinari, mpaka nyumba ya mungu wake; akaviingiza vile vyombo katika nyumba ya hazina ya mungu wake.
3 Mfalme akamwambia Ashpenazi, mkuu wa matowashi wake, awalete baadhi ya wana wa Israeli, wa uzao wa kifalme, na wa uzao wa kiungwana;
4 vijana wasio na mawaa, wazuri wa uso, wajuzi wa hekima, werevu kwa sababu ya maarifa yao, wenye kufahamu elimu, watakaoweza kusimama katika jumba la mfalme; tena alimwambia awafundishe elimu ya Wakaldayo, na lugha yao.
5 Huyo mfalme akawaagizia posho ya chakula cha mfalme, na ya divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.
6 Basi katika hao walikuwapo baadhi ya wana wa Yuda, Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria.
7 Mkuu wa matowashi akawapa majina; alimwita Danielii, Belteshaza; na Hanania akamwita Shadraka; na Mishaeli akamwita Meshaki; na Azaria akamwita Abednego.
8 Lakini Danielii aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.
9 Basi Mungu alimjalia Danielii kupata kibali na huruma machoni pa huyo mkuu wa matowashi.
10 Mkuu wa matowashi akamwambia Danielii, Mimi namwogopa bwana wangu, mfalme, aliyewaagizia ninyi chakula chenu na kinywaji chenu; kwa nini azione nyuso zenu kuwa hazipendezi kama nyuso za vijana hirimu zenu? Basi kwa kufanya hivyo mtahatirisha kichwa changu mbele ya mfalme.
11 Ndipo Danielii akamwambia yule msimamizi, ambaye mkuu wa matowashi amemweka juu ya Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria,
12 Tafadhali utujaribu sisi watumishi wako muda wa siku kumi; na watupe mtama tule, na maji tunywe.
13 Kisha nyuso zetu zitazamwe mbele yako, na nyuso za wale vijana wanaokula chakula cha mfalme; ukatutendee sisi watumishi wako kadiri ya utakavyoona.
14 Basi akawasikiliza katika jambo hilo, akawajaribu siku kumi.
15 Hata mwisho wa zile siku kumi nyuso zao zilikuwa nzuri zaidi, na miili yao ilikuwa imenenepa zaidi, kuliko wale vijana wote waliokula chakula cha mfalme.
16 Basi yule msimamizi akaiondoa posho yao ya chakula, na ile divai waliyopewa wanywe, akawapa mtama tu.
17 Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danielii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
18 Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadreza.
19 Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danielii, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.
20 Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.
Wayahudi walitenda dhambi na Mungu aliwakemea lakini hawakusikia. Kawaida Mungu kabla ahajakuletea jambo anakupa taarifa kwanza mabaya yata kupata kama wana wa Israeli walikemewa na Mungu lakini hawakusikia ndiomaana walipelekwa utumwani miaka sabini na hili kwenye maisha yetu hata kama utalia kiasi gani lazima adhabu Mungu aliyoipanga baada ya kukuonya ukakataa lazima itimie.
Danieli alipogundua ile miaka sabini imetimia ya adhabu ya Mungu akaamua kuanza kutubu na kuomboleza kwa niaba ya Israeli wote, ukitaka kuwa mwombaji mzuri hakikisha unamwomba Mungu msamaha unaomba msamaha kwaajili ya familia yako, ndugu zako, rafiki zako taifa lako. Alipomaliza kumwomba Mungu msamaha Mungu alimfungulia njia ya kurudi walipotoka.
Inawezekana kuna mabaya ambayo yalipangwa yakupate lakini unapomwomba Mungu msamaha anakufungulia njia ukafanikiwe kwenye safari, ndoa, bihashara, kazi, elimu na mambo mengine.
Yeremia5: 25 Maovu yenu yameyageuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate.
Yeremia2: 19 Uovu wako mwenyewe utakurudi, maasi yako yatakukaripia; ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi.
Mithali28: 13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.
Ukiungama dhambi alafu ukaziacha sio kusema tu Mungu naomba unisamehe je unamwomba Mungu msamaha leo alafu uzirudie kesho? Njia la kupata rehema ni kuziacha dhambi zetu zote.

Dhambi ya mtu inaweza kumzuilia mtu asipate mema,
Zaburi 103: 3 Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
Mungu anaweza kukusamehe maovu yako yote na kukuponya magonjwa yako yote
Zaburi32: 1 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.
Neno heri maana yake ni Baraka na kumbe Baraka zinaanza kwenye msamaha wa dhambi. Msamaha wa dhambi ni wa hakika na unaleta baraka
Isaya43: 25 Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.
Mungu anapokusamuehe wala hakumbuki kama ulikosea hapo nyuma ‘Mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya yakale yamepita’.
Isaya44: 22 Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.
Yeye afichaye dhambi na kuziacha atafanikiwa na aziungamaye na kuziacha atapata rehema, Mungu anasema kwakuwa nimekusamehe hata hayo usiyostahili kuyapata chukua
Mathayo9: 2 Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako.
Yesu anasamehe dhambi pia
Marko2: 25 Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa ana haja, na kuona njaa, yeye na wenziwe?
Luka5: 20 Naye alipoiona imani yao, alimwambia, Ee rafiki, umesamehewa dhambi zako.
Lika7: 48 Kisha alimwambia mwanamke, Umesamehewa dhambi zako.

Mema yanatujia baada ya kusamehewa dhambi, na mwaka huu ni mwaka wa kutiisha, kumiliki na kutawala itakuwa vile vile kama alivyosema Bwana na huwezi kutiisha, kumiliki na kutawala bila kusamehewa dhambi lazima utubu ili upate kusamehewa dhambi zako na upate rehema za Mungu kwenye maisha yako kwa jina la Yesu.
Mungu hunyanganya watu waovu mali zao na kuwapa wenye haki. Mungu ni Mungu wa kuongea na kutenda baadaye.
Yona1: 1 Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema,
2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
3 Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana.
4 Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
5 Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi.
6 Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini, Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
7 Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na mpige kura, mpate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona.
8 Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani?
9 Akawaambia, Mimi ni Mwebrania; nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeziumba bahari na nchi kavu.
10 Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha.
11 Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itulie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka.
12 Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itatulia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata.
13 Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana.
14 Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.
15 Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.
16 Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri.
17 Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.
Yona2: 1 Ndipo Yona akamwomba Bwana, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,
2 Akasema, Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu naliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.
10 Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.
Yona aliambiwa na Mungu akahubiri ninawi akakataa na kwenda mji wenye raha tarshishi hivyo akamtenda dhambi Mungu. Kila mtu ametumwa na Mungu na kukatazwa kutokufanya kitu Fulani akakataa mtu anajidai ana nyumba, ana gari, ameolewa hataki kumsikiliza Mungu unakuta mtu wa namna hiyo akiamua kufanya jambo anatumia nguvu kubwa na unakuta wakati huo Mungu anatuma jambo likuzuie kile unachokifanya na mabaya yanampata kwasababu hiyo.
Walimwona Yona amelala wakaamua kupiga kura ili wajue mabaya yale yamewapata kwasababu gani na kura ikamwangukia Yona walipo muuliza akawaambia ameukimbia uso wa Bwana, kumbe mtu anaye mcha Mungu aliyeokoka anapotenda dhambi upepo unavuma na kunatokea dhuruba kwenye maisha yake iwe ni elimu au buhashara au ndoa kwenye maisha ya mtu huyo.
Unapokuwa dhambini iwe ni bihashara kubwa aundogo inakuwa ngumu, iwe ni kazi kubwa au nyepesi inakuwa ngumu kwasababu ya dhambi hiyo.
Yona alipotupwa baharini bahari ilitulia na kwenye maisha yetu ukiliondoa bahari inatulia iwe ni bahari ya familia, bahari ya bihashara, bahari ya uchumba, bahari ya madeni, bahari ya umasikini. Yona alifunga tumboni mwa samaki siku tatu usiku na mchana mpaka akakuita kuzimu, kwaajili ya makosa yetu tumeomba siku ya tatu leo na Mungu ametuona tumebadilishwa muelekeo, ulitakiwa kufa utaishi, ulitakiwa kuvunjika mguu umebadilisha muelekeo na leo tumetapikwa tunamwambia Bwana tupo tayari kubadilisha muelekeo kwasababu Bwana amemwamuru samaki wa mateso atutapike na turudi kuyatenda yale tuliokataa kuyatenda.

Samehe wote waliokutendea dhambi kwenye maisha yako yote kutoka ndani ya moyo wako ili Mungu Baba wa Mbunguni akusamehe na upate rehema na Amani ya moyoni kwa jina la Yesu.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.