SOMO: TAFUTA KUJUA NAMNA YA KUSHUGHULIKIA MALANGO YA MJI WAKO.- Sehemu ya mwisho.Bwana Yesu asifiwe sana…

Karibu katika siku ya leo ambapo tunakwenda kumalizia kwa ufupi sana juu ya kile tulichokuwa tukijifunza mahali hapa.
Kumbuka,milango ya mji wako ipo kiuharisia na wala sio hadithi tu. Wengi leo wanateswa na nguvu za mizimu,wengine huteswa na magonjwa yenye kufanana katika familia,sasa haya yote na mengine huja kwa sababu ya milango iliyo wazi yenye kupitisha au kusimamisha uharibifu.

Mfano mzuri ulio hai ni huu hapa;
Hivi karibuni nimepokea ujumbe wa mtu ambaye anasumbuliwa na nguvu za mizimu. Mizimu ya ukoo wao inamtesa sana,tena isitoshe mtu huyo sio kana kwamba hajaokoka,la hasha! Ameokoka,na ni mtumishi wa Mungu.

Sasa ikiwa mtumishi wa Mungu anasumbuliwa na nguvu ya mizimu,maana yake hata wewe unaweza kusumbuliwa na nguvu hiyo hiyo iliyotoka katika lango la ukoo wa kwenu.Na ndio maana nakuambia kwamba mambo haya yapo kiuharisia hata kama wewe labda hupitii katika shida hizi.
Chanzo chote cha mateso ni kutoshughulikia lango la mji wako.

Tena wapo watu ambayo lango la mji wake lina madai na yeye,yamkini alikabidhiwa kwa wachawi angali akiwa mdogo pasipo yeye kujijua,na anashtuka akipitia katika msoto wa mateso katika maisha yake ya sasa.

Kumbuka jambo hili,
Waweza kujiuliza kwamba mbona mimi nimeokoka sasa haya yote ni ya nini ?
Yaani nitawezaje kusota na nguvu za mapepo katika familia au ukoo wangu hali mimi nimeokoka ?

Lakini kumbuka pia;
Ukiokoka unapewa uwezo wa kuyashinda hayo yote. Neno ” kuyashinda ” maana yake ipo vita,sababu huwezi kushinda pasipo vita,panapo vita ndipo panapo kushinda. Na kama ipo vita maana yake unatakiwa wewe uliyeokoka upigane katika ulimwengu wa roho huku ukiwa tayari umeahidiwa ushindi katika hiyo vita,sababu biblia inasema tunayaweza mambo yote katika Kristo Bwana ( Wafilipi 4:13 )

Sasa ile namna ya kupigana,ndio hii tunayojifunza sasa.
Tunachohitaji kujua ni namna ya kushughulikia malango yaliyo wazi katika miji yetu,ili tuyafunge kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,malango hayo yasipitishe tena maovu.

Wapo wakuu katika familia au ukoo ( Malango ) waliokufa lakini malango yao yapo hai mpaka sasa. Malango kamwe hayakufi kwa kufa kwake mwenye lango,bali akifa mkuu huyo malango hubakia wazi. Malango haya yanaweza kupitisha vitu vibaya mpaka sasa.
Adui ili awapige katika mji wako,hutafuta mahali penye lango,la sivyo hawezi kuingia na kuwapiga.

Ngoja nikupe mfano kidogo,
Ili mwizi aibe vitu vyako vya chumbani,basi ni lazima atatafuta ni wapi penye mlango wa chumba ili afanikishe zoezi lake. Laiti kama utafanikiwa kuufunga vizuri mlango wako basi ni dhahili mwizi hawezi kuingia kabisa na hatimaye utakuwa salama.

Alikadhalika ni vivyo hivyo katika malango ya miji yetu,shetani adui hutafuta mahili penye lango la wazi aingie na kuupiga mji wote.

Sikia mfano mwingine huu;

Mtu mmoja alienda bafuni kuoga,si unajua tena yale mabafu ya nje ya nyumba. Alipoingia bafuni akajisahau kufunga mlango wake wa chumbani,kisha akaenda kuoga.Kabla hajaanza kujimwagia maji,yaani ile ameingia tu bafuni.
Ndipo hapo hapo mwivi naye akaja na kuingia chumbani. Dakika chache kabla ya kuanza kuoga akakumbuka ya kuwa mlango wa chumbani kwake upo wazi,akakimbia akaufunga kisha akaanza kuoga pasipo kujua kwamba amemfungia mwizi ndani ya chumba chake.

Aliporudi,akaufungua kisha akaingia ndani na kuufunga mlango tena na kuhakikisha ameufunga sawa sawa,na funguo ikabaki katika kitasa,akalala. Alipoamka asubuhi alikuta baadhi ya vitu vyake vya chumbani vile vidogo vidogo vimeibiwa mfano simu,lap top N.K

Akaanza kujiuliza kwamba huyo mwizi kaingiaje ? Maana mbona aliufunga mlango!! Hakupata jibu wala hakukumbuka kabisa kwamba pale alipojisahau kidogo tu bafuni ndipo mwizi aliingia katika mlango wa chumba chake.

Kumbe!
Pale unapojisahau kidogo tu,ndipo hapo hapo unapompa mwanya adui aingie na kukupiga. Katika miji yetu,kupo hali ya kujisahau kuombea,kupo hali ya kupuuzia mambo haya,kupo hali ya kutokujua vizuri mambo haya,na yote hayo ndio mianya inayomruhusu adui aingie na kufanya uharibifu.


Mtumishi wa Mungu Gasper Madumla.

Njia ya pekee ya kushughulikia milango yate iliyo wazi,ile yenye kupitisha uovu,ni njia hii;
●Kuifunga milango ya miji kwa damu ya mwanakondoo aliye hai yaani kwa damu ya Yesu Kristo pekee.

~ Ndani ya damu ya Yesu Kristo kuna uweza wa ajabu wa kuulinda mji na malango yeke yote,pasipo kujalisha ni lango la aina gani yaani iwe ni lango la ufukara,au iwe ni lango la laana,au iwe ni lango la magonjwa,au iwe ni lango la kukataliwa- Yote hayo yanafungwa na kusafishwa kwa damu ya msalaba,damu ya Yesu Kristo.

Niseme nini tena hapo!
Ikiwa damu ya Yesu inasafisha kila kitu.

Tazama wana wa Israeli,waliambiwa waipange miimo ya malango ya nyumba zao kwa damu ya mwanakodoo kumzuia yule mwenye kuharibu asiharibu ( Kutoka 12:22 )
Damu ya Yesu imethibitishwa na Mungu mwenyewe,mimi nina uhakika nayo asilimia zote,sina shaka nayo hata kidogo sababu ipo hai na inaishi na kufanya kazi hata sasa.

Mpendwa nakushauri bure,ikiwa hutaki tena kuona mateso katika familia yako yakiendelea,mateso katika ukoo wako,mateso kwa watoto wako N.K Basi hauitajiki kwenda mahali popote pale kwa wanadamu wa kawaida ili wakupe dawa sababu hawana dawa ya sampuli hiyo.

Bali dawa ni Yesu mwenyewe,unahitajika kuliendea jina la Yesu Kristo likuokoke,uokoke kwa kukukupa maisha mapya wewe,kisha kwa damu yake BWANA unaitumia kwa kusafisha malango ya mji wako. Nayo yatakuwa safi.

Kwa huduma ya maombi na maombezi,tafadhali sana unipigie ili tuyafunge hayo malango ya giza katika familia au ukoo wako.
Nipigie katika namba yangu hii;
0655~11 11 49.

UBARIKIWE.
MWISHO.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.