SOMO: UMEANGUKA UMEANGUKA EWE BABELI
SOMO: UMEANGUKA UMEANGUKA EWE BABELI - MCHUNGAJI PAUL JOSHUA 

Bustani ya edeni ilikuwa babeli ambapo sasaivi panajulikana kama Iraq
Mwanzo 2:7-15
Hapo awali hapakuwa na bustani wakati Adam anaumbwa, lakini Mungu alipanda bustani nzuri pembeni ya edeni, bustani haikuwa ndani ya Eden ila ilikuwa pembeni ya Eden,nakulikuwa na mito ambayo ilimwagilia bustani hiyo,

Kuna vitu ambavyo shetani amevificha baada ya Adamu na Eva kuanguka akajimilikisha utajiri wote na kwahuo waganga wa kienyeji na wasoma nyota wanawapatia wateja wao maana shetani hana kitu wala hajawahi kuumba,hivyo anatumia mali alizojimilikisha pale edeni kudanganyia watakatifu wa Baba, hapo alijaribu kumdanganyia hata Yesu yakuwa akimuabudu atampa milki zote lakini kiuhalisia hana chochote ila aliiba/alijimilikisha mali zote pale Edeni. 

Nchi zote za kiarabu zilikuwa nchi za kikristo kam vile Iran, Iraq n.k lakini sasa hivi zimekuwa nchi za kiislamu maana babeli huyu kajimilikisha. Ndio maana utaona majini yote asili yake ni uarabuni maana ndiko mwanamke huyu kahaba anaachilia roho kutetketeza watoto wa Yesu
Bustani ya edeni hii ndio ilikuwa imejengwa babeli ambapo leo inajulikana kama Iraq

Ufunuo 17:1-6
Huyu mama kahaba kanywa damu za watakatifu na mashahidi wa Yesu mpaka kalewa ,mama huyu haangalii mtume wala mwinjilisti wala nani; ukikaa vibaya huyu mama anakumaliza,vilevile huyu mama anakazi ya kushindana na kanisa, anatuma na anaachilia roho ambazo zinaangusha watumishi wengi wa YESU. Ndio maana watumishi wengi wameanguka kwa uzinzi na sio wizi,wala ulevi maana mama huyu ameachilia roho za ukahaba ambazo zinawafuatilia watakatifu wa BWANA na mashahidi wa Yesu yaani wachungaji , wainjilissti , mitume,

Ufunuo 18:1-12
Yohana aliendelea kuoneshwa maono. Alioneshwa babeli anaanguka chini, mamahuyu ameangusha wafanyabiashara wa nchi, maraisi, na wafanya biashara. Wananchi wamepata utajiri kwa nguvu za kiburi chake.
Yeremia 50:24-25.
Huyu mama amekunywa damu za watakatifu na Mungu ameamua kumtega, naye anashida na wakristo, huyu mama anashindana na BWANA ,anashindana na Mungu wetu,ameshiba damu ya watakatifu na anakiburi sana

Ufunuo 18:15
Mama huyu alichukua utajiri wote katika bustani ya edeni ambao Adam alipewa na Mungu na ndio huo anawagawia wafanyabiashara wanchi,kila aliyefanikiwa elewa kuwa kuna nguvu ya rohoni inayomfanya asonge mbele ,kama sio Mungu basi ya shetani(mganga wakienyeji) ndio maana kila unayemuona kastawi kwa hali yoyote ile anaye ambaye anamtegemea katika ustawi huo.

Ufunuo 17:18 mwanamke huyu unayemuona ni mji ule mkubwa wenye ufalme juu ya wafalme wanchi, mama huyu ndiye anayeongoza wafalme wa nchi(maraisi) ni hatari sana kuwa na mfalme asiyenaYesu (aliyeokoka) maana kwa namna yoyote huyu mama lazima amtumikishe kwakuwa yeye ni mfalme juu ya falme, na wafalme wote hufanya mambo kwakuongozwa na mama huyu kahaba.
Zaburi 2:2-3 wafalme wa dunia wanajipanga , na wakuu wanafanya shauri pamoja , juu ya bwana na juu ya masihi wake. Natuvipasue vifungo vyao, na kuzitupa mbali nasi kamba zao.
A M E N.

Mchungaji Paul Joshua- Ufufuo na Uzima

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.