USHAURI KWA WALOKOLE WENZANGU - MASANJA


Mnaosoma someni kwa bidii hasa, mliomaliza tafuteni cha kujiajiri kuliko kuajiriwa mda unaoupoteza ukisubiri kujiriwa unaweza ukawa mbali ktk maishaa,

Wadada acheni kuwaza ndoa kuliko kazi ya kukupa kipato, mume wako yupo tuu sehemu usikurupuke kisa wenzio wanaolewa, kwa umri wako piga kazi kijana akukute unamaisha yako hata unahamia kwa mme wako unakodi fuso ya kubebea vitu ulivyojitafutia lazima mme akuheshimu kuwa wewe ni jembe!!

Unataka uende kwa mmeo na kamfuko tuu ka malboro hata mawifi hawatakuheshimu, kuwa mdada wa kitanzania jishughulishe sio full time upake kucha rangi za mikono na miguu, yaan hata nguo unafua kama mlemavu kisa makuchaaaaa!!

Na sisi vijana kuwa na chumba cha kulala na godolo jipya sio kigezo cha ndoa, mwanamke anahitaji kuhudumiwa so chomolea shati vaa pensi kapige kazi maisha yaendelee ukiona siku inaisha hauna hata faida ya 2000 jipange upya.

Mwisho tujichanganye bila kuogopa, kama unauwezo wa siasa chukua jimbo unauwezo wa kuimba ingia studio unauwezo wa kucheza piga step za kufa mtu labda hapo ndipo ulipoitiwaaa

Mwisho tujifunze ku view international ulokole wa tanzania ukiuendekeza hutaweza kuabudu nchi za watu, jiamini wokovu upo ndani yako sio midomoni mwa watu mwisho unakuwa pritendaaaaaaaaaa jst because unataka kuridhisha watu

2015 ni mwaka wa furaha usiruhusu mtu akuletee huzuni moyoni mwako.

Asanteni naomba kuwakilishaa!!!
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.