CHAGUO LA GK KAMA HUNA ALBUM HII UNAKOSA JUMBE ADIMU SANA KATIKA MUZIKI WA INJILI NCHINIChaguo la GK leo ni kukukumbusha tu kwamba kama hauna toleo la kanda hii basi unakosa jumbe adimu sana katika medani ya muziki wa injili nchini. Kama kuna kwaya ambayo nyimbo zake huwa zinawasogeza watu karibu na Mungu, kutokana na tafakari kuu zinazoimbwa basi Tumaini Shangilieni Kwaya St James Arusha haina mpinzani kwa nyimbo za tafakari na toba.

Mapema mwaka jana walitoa video mpya iitwayo 'Nisamehe' kupitia video hiyo tumekuchagulia nyimbo mbili ambazo binafsi zinanibariki sana kuanzia muziki mpaka maneno, nina uhakika zitaifanya jumapili yako kuwa njema na kama huna toleo lao basi utatafuta ili umiliki nyumbani kwako. Katika chaguo tumechagua wimbo uliobeba kanda uitwao Nisamehe na wimbo wa pili unaitwa Niongoze Bwana.
Tunakutakia baraka za Mungu utazamapo na kusikiliza nyimbo hizi ambazo zinafanyika baraka kwa watu wengi waliopata kuzisikiliza.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.