CHAGUO LA GK NI PAMBIO KUTOKA WASHINDI WA KOMBE LA AFRIKA

Kundi la Schekina. ©Kanayokib blog
Tunatumai u mzima mdau wa Gospel Kitaa kwa Jumapili ya leo. Chaguo la GK tarehe 15 Februari 2015 linatoka kwa washindi wa kombe la mataifa ya Afrika, Ivory Coast. Hapa tunakutana na kundi liitwalo Schekina, ambalo limeundwa mwaka 1999.

Kwa pamoja wimbo wao ulio pambio maarufu kwa Kiswahili, Hakuna Mungu kama wewe. Lakini hapa wameimba kwa lugha ya kwao, kifaransa, wakisema, "Personne comme Jésus".

Tunakutakia Jumapili njema yenye baraka tele, lakini kati ya yote, hakuna na hatakuwepo kama Yesu duniani kote, hivyo chochote umuombalo ni kwa hakika anasikia na atakutendea sawasawa na mapenzi yake. Usichoke kuongea naye.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.