CHAGUO LA GK VIDEO MPYA YA INJILI KUTOKA KWA MTANZANIA, TAYARI IMEOMBWA NA VITUO VYA KIMATAIFAChaguo la GK siku ya leo ikiwa jumapili ya kwanza mwezi February, tumekuchagulia video mpya kabisa iliyotoka wiki hii kutoka kwa mwanakaka Warren Bright mwimbaji wa nyimbo za injili nchini na muumini wa kanisa la Sabato la Ushindi Mikocheni jijini Dar es salaam. Warren ni kiongozi wa kundi la Voices of Victory pia ni mume wa Claire Humure mwimbaji wa kwaya ya Kwetu Pazuri ya Rwanda.

Tumekuchagulia video hii ambayo tayari imeleta habari njema kwa mwimbaji husika lakini pia kwa tasnia ya muziki wa injili nchini kwa ujumla kwani video hiyo imeingizwa kwenye kinyang'anyiro cha mwimbaji bora wa Africa kwenye kipengele cha video za kimataifa yaani za viwango.Lakini pia ili video hii ili ionyeshwe kwenye vituo vya kimataifa kama 3ABN, TBN pamoja na Channel O, itahitajika iwe imetizamwa mara 5000 kwenye mtandao wa YouTube kazi ambayo naamini ni rahisi sana kwa watanzania wote.Video ya wimbo 'I'm on my Way' ya Warren Bright ambayo imerekodiwa na kampuni ya Eliel Filmz ambao pia wamerekodi album mpya ya Ibatebuli ya kwao Ambassadors of Christ Rwanda, hakuna ubishi kwamba ipo kwenye viwango. Shime kwa watanzania unaweza kuitazama video mara nyingi uwezavyo ili kuhakikisha tunafikisha kutizamwa mara 5000. Jumapili njema

Warren na mkewe Claire


Haya ni maneno yake Warren kupitia ukurasa wake wa Facebook

Wapendwa, nimepokea Habari njema sana kwangu kutoka DSTV Mult Choice about my new Video I'm on my way, Video hiyo imewekwa nominated katika African Gospel Artist International Videos, ili iweze kuchezwa katika vituo vya 3ABN,TBN na Channel O, In YouTube nahitaji kupata views 5000 tu Ndani ya Mwezi mmoja tu FEBRUARY, Success comes when you focus on it, dear friends naomba mzidi kutembelea link ya YouTube wewe na marafiki zako kuwezesha my video kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya kimataifa.Link hiyo ni: https://m.youtube.com/watch?v=rPH7UQatoOs
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.