HAPPY BIRTHDAY SILAS MBISE

Sila na rafikize mtaani
Siku na saa zinakwenda, lakini kwa hayo tunamshukuru Mungu, maana tokea ukiwa mdogo umefanyika baraka kwa wanakuzunguka. ilikuwa juzi tu yaani namaanisha mwaka jana tulipokutakia heri ya kuzaliwa mara hii tena ka mwaka kameisha umeongeza mwaka mwingine wa kutumika katika shamba la Baba yetu wa Mbinguni.

Sio siri kijana Mungu amekukirimia vipawa mbalimbali ambavyo kwavyo umeendelea kufanyika baraka shambani mwake. Team GK inafurahi kuwa nawe katika kulisongesha hili gurudumu la Injili licha ya majukumu mengi tuliyonayo lakini GK ni moja ya jukumu zito na kubwa ambalo tunalipa kipaumbele kwa pamoja.

Mungu aliyekujua toka misingi ya dunia haijaumbwa tunamuomba Rehema zake ziendelee kuambatana nawe na kila ahadi aliyosema juu maisha yako akapate kuitimiliza ili watu tunakapate kufaidika kwayo. Happy Birthday Silas, mwaka ulioongeza leo ulete majibu ya yote uliyokuwa ukiyaomba miaka iliyopita. Ubarikiwe.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.