HATIMAYE KEKE AFUNGA NDOA YAKE YA TATU AWEKA PICHA HEWANI

Hatimaye mwimbaji nyota na nabii Kekeletso Phoofolo ama kwa kifupi Keke wa nchini Afrika ya kusini amefanikiwa kufunga ndoa yake ya tatu na kuweka baadhi ya picha katika ukurasa wake wa Facebook na kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa ndugu, jamaa, marafiki pamoja na wanaosapoti huduma yake.

Mwimbaji huyo ambaye pia ni nabii ndoa zake mbili za mwanzo zilikumbwa na upepo kabla ya kuamua kuoa tena kwa mara ya tatu hivi majuzi na tayari yupo mbioni kuachia album mpya. Keke amefanikiwa kuwagusa watu wengi ndani na nje ya nchi yake linapokuja suala la kuimba nyimbo za kusifu, huku wimbo wa Che che che ndio ulitokea kupendwa sana. Lakini linapokuja suala la ndoa, ameonekana kushindwa kuakisi taswira ya huduma aliyonayo. Keke ni baba wa watoto watatu. Kusoma habari zaidi juu ya ndoa zake nyingine bonyeza hapa
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.