KAZI IMEANZA ILA MSAADA WAKO BADO WAHITAJIKAHatimaye baada ya mwamko kutoka kwa wasomaji wa Gospel Kitaa katika kuchangia ujenzi wa kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo kijiji cha Kidogo basi huko wilayani Kilosa mkoani Mororgoro ujenzi huo umeanza huku mchungaji kiongozi akiomba msaada zaidi ili kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo.

Katika habari tuliyoandika mwezi November mwaka jana yenye kichwa  "SIMBA WA YUDA AUNGURUMA KILOSA, WATU 30 WATOKA KWENYE UISLAMU, MSAADA WAHITAJIKA"ili ibada ziweze kufanyika katika hali ya uchaji na usalama zaidi hasa ukizingatia katika kijiji hicho kuna misikiti zaidi ya nane. Ambapo watu mbalimbali waliweza kuitikia mwito huo kwa kuchangia kidogo. Hata hivyo mchango huo haujatosha hivyo mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo  ameomba watu kujitokeza zaidi kuchangia ujenzi wa kanisa hilo.

Ili kuchangia pamoja na kuwasiliana na mchungaji tumia namba hii 0685863454

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.