KWA TAARIFA YAKO: USICHOKIJUA KUHUSU MWALIMU WA KWAYA YA KWETU PAZURI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo kwa mara nyingine tupo nje ya Tanzania ingawa muhusika anafahamika vyema nchini kutokana na kazi nzuri anayoifanya pamoja na kundi analoliongoza.Kipengele chetu hii leo kinataka kukufahamisha kuhusiana na mwalimu wa kwaya ya Ambassadors of Christ ya Rwanda ambao wametamba na wimbo wa 'Kwetu Pazuri' bwana Ssozi Joram.KWA TAARIFA YAKO kama hufahamu ni kwamba mwalimu Ssozi Joram ambaye pia maeanzisha nyimbo mbalimbali katika kwaya hiyo ukiwemo wimbo kama Moyoni mwangu ninashukuru na nyinginezo. Ni Mganda na si Mnyarwanda kama wengi wanavyodhani. Mwalimu Joram alijiunga kufundisha kwaya ya Ambassadors nchini Rwanda mnamo mwaka 1998 akitokea kwao nchini Uganda ambako pia alikuwa akijihusisha na masuala ya muziki akiwa mtayarishaji wa muziki katika studio ya Jameni ambayo ipo maeneo ya Chikoni jijini Kampala nchini Uganda na ndio maana ukisikiliza nyimbo nyingi za kwaya hiyo zina midundo ya Kiganda.
KWA TAARIFA YAKO mwalimu huyo ambaye pia ameshiriki katika kutungia nyimbo kwaya na vikundi vingine inaelezwa amebarikiwa sana linapokuja suala la utungaji, muziki na namna ya kuifanya kwaya kuimba kwa sauti zilizopatana na nyimbo zenye mtiririko uliopangiliwa vyema kama ilivyo kwa nyimbo za kwaya ya Ambassadors of Christ ambao kila mwaka hutoa album mpya huku pia ikiwa na waanzilishaji tofauti wa nyimbo tofauti na kwaya nyingine.
KWA TAARIFA YAKO mwalimu huyo ameitengeneza kwaya ya Ambassadors of Christ kutotegemea mtu mmoja katika uimbaji na hilo limewezekana kama inavyoonekana katika matoleo mbalimbali ya kwaya hiyo. Joram aliweka wazi siku moja akiwa anahojiwa kwenye kipindi cha Lulu za Injili kinachorushwa na radio ya kisabato jijini Dar es salaam ya Morning Star kwamba kila mwimbaji wa kwaya hiyo anafundishwa kujua kuanzisha nyimbo sawa na ilipokuwa solo wao wa zamani amabye kwasasa amerejea kwenye kwaya aitwaye Mbabazi Milly alikuwa akianzisha nyimbo nyingi za kundi hilo na mara alipoacha mwanadada Yvonne Matilda Umunyana ama malkia wa Kwetu pazuri aliweza kushika kundi vizuri na mara alipopata likizo ya uzazi kuna waimbaji wengi walioshika nafasi yake vyema kama Sara Uwera kipenzi cha wengi kwasasa, Ngamije, Claire anayeishi nchini kwasasa bada ya kuolewa na Mtanzania na waimbaji wengine wengi.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.