KWA TAARIFA YAKO: KUTOKA 'DISKO' HADI UABUDU, NEW LIFE BAND ILIVYOVUKA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Deo, Ondo na Gideon kwenye tamasha la Krismasi jijini Dar es Salaam, 2013.
Huduma ya Mission to Youths si ngeni masikioni mwa watu, lakini ilikuwa ngumu sana kipindi hicho ukizingatia kwamba New Life Band wanakaribia umri wa miaka 40. KWA TAARIFA YAKO mojawapo ya ugunu walioupata kipindi wanaanza huduma hii ni pamoja na kuitwa wapiga disko. Hilo KWA TAARIFA YAKO ikiwa ni kutokana na kuwa watu wa kwanza kuingiza ngoma kanisani. Hiyo ngoma ikawa na mapokeo tofauti kwa watu mbalimbali ikiwemo mchungaji wa kanisa fulani mkoani Iringa, ambaye aliifananisha na muziki wa disko. Na mara baada ya kuondoka kuendelea na huduma mahala pengine, huo ndio ukawa mwisho wa ngoma hiyo kuwepo kanisani. Iliondolewa.

Tofauti na siku hizi, ambapo kumekuwa na mitindo ya kila aina ili mradi sifa na utufuku zimrudie Mungu, kipindi cha miaka ya 70 ilikuwa tofauti sana, kwani KWA TAARIFA YAKO kucheza ilikuwa ni jambo gumu, sembuse kurukaruka.

New Life Band ambayo ina umri wa takriban miaka 37 sasa (miaka 36 kwa mujibu wa ukurasa wa facebook, New Life Band MTY) imepitia mengi sana hata kufikia sasa ambapo wao wanaitambua huduma ya uimbaji kama yenye nguvu kuliko hata mahubiri, kwa kuwa uimbaji upo kila sehemu. Hivyo basi ni muhimu kwa waimbaji kufahamu umuhimu wa tasnia waliyonayo, na hata kutoipoteza nafasi ambayo Mungu amewapa kwa ajili ya kuhubiri.

Mr & Mrs Ondo
KWA TAARIFA YAKO pamoja na yote ambayo muimbaji ambayo utafanya, kitu kimopja ambacho kinawaangusha waimbaji wengi ni kiburi, baada ya kuona kama wamekubalika. Shetani ndio mfano bora kwenye hilo. New Life Band wameonesha mfano kwenye hili, na ndivyo ambavyo wana shauku ya kuona waimbaji wengine wote wakinyenyekea.

Aidha kwa mujibu wa Bwana Ondi, ambaye ndiye mbeba maono wa New Life Band, anaeleza kwamba pamoja na huduma hii kuanza enzi hizo akiwa kijana mdogo, kitu muhimu cha kuzingatia ni kuhakikisha kwamba ujana wako haudharauliwi. Hii ni pamoja na kutoanya mambo ambayo yatapelekea wewe kudharauliwa na ujana wako. Kuanzia mavazi na hata aongea yako.

Hiyo ndo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.