KWA TAARIFA YAKO KWAYA MAARUFU YA KILUTHERI NCHINI YENYE UIMBAJI WA KIPENTEKOSTE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo jijini Dar es salaam, ambako tutazungumzia kwaya moja iliyojibebea umaarufu kwasababu ya wimbo wao mmoja tu ambao uliwafungulia mlango wa kujulikana katika huduma yao ndani na nje ya nchi. Kwaya hii ilikuwa ni kwaya pekee mwishoni mwa miaka ya 80s kutoka kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT) kujulikana na kualikwa kwenye mikutano mikubwa ya injili.

KWA TAARIFA YAKO nazungumzia kwaya maarufu ya Uinjilisti Mtoni ama waite Lulu Mtoni, kwaya hii iliweza kupenya masikioni mwa watu baada ya kutoa kibao chao cha 'Lulu' wimbo ambao ulikuwa miongoni mwa nyimbo za kwaya kwa miaka hiyo kupendwa zikiwemo nyimbo za kwaya ya Victory Singers kutoka kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Revival Kinondoni pamoja na Rhema Singers kutoka TAG Mnazi mmoja zote za jijini Dar es salaam.
KWA TAARIFA YAKO uimbaji wa Lulu katika mwendelezo wa kanda zake kwa mtu aliyezisikiliza kwa mara ya kwanza ama hajasoma picha ya kanda ya kwaya hiyo akisikia namna ya uimbaji wao ulivyo akili yake moja kwa moja itamwambia hiyo kwaya ni kutoka kanisa la TAG ama Pentecoste kwasababu ya namna ya uimbaji wao haujajishikiza kwenye sauti za namna kwaya za kanisa la Kilutheri Tanzania zinavyoimba. 

KWA TAARIFA YAKO ukisikiliza wimbo kama Tazameni, Yesu ni mzuri, Haleluya ni moja kwa
Marehemu George akiwa na Lulu katika moja ya huduma

moja huwezi kudhani ni kwaya ya Kilutheri kwamaana asilimia 90 za kwaya za kanisa hilo wanaimba kufuatisha utaalamu wa kimuziki zaidi (naomba nieleweke, kuna namna kwaya za Kilutheri zinavyoimba ni tofauti kwa Lulu) kunielewa zaidi sikiliza moja ya nyimbo nilizozitaja hapo juu. Kwaya hii ya Mtoni Mtongani jijini Dar es salaam moja ya sifa zake ni kwamba inaweza kumshambulia adui haswa ukutanapo nao wanakuwa kazini zaidi, wanaimba kwa hisia ikiwa pamoja na kufurahia kile kitokacho mdomoni mwao.
KWA TAARIFA YAKO uimbaji wa Lulu niwa kipekee kwanza ni moja kati ya kwaya katika kanisa la Kilutheri wanaofanya maombi sana juu ya huduma yao, lakini pia walimu na timu yao ya wanamuziki walikaa pamoja kwa muda mrefu ikiwa pamoja na wapendwa wao waliotangulia mbinguni siku za hivi karibuni. KWA TAARIFA YAKO nilipata wasaa wakusikiliza album mpya ya Lulu ambayo kwakawaida ilitakiwa kutoka miaka kama minne iliyopita kwakuwa hata WAPO Radio FM ilishafikishwa na kupigwa siku moja kabla ya mwalimu wao ambaye kwasasa ni marehemu hakutaka kanda itoke kwakuwa hakuridhishwa na kiwango cha kanda hiyo. Sahau kuhusu hilo ila ninalotaka kukwambia ni kwamba nyimbo zilizomo katika album hiyo ni mwendelezo wa uinjilisti zikiwa zimejaa neno, lakini pia mtiririko wake ni mwendelezo wa Lulu iliyojitambulisha toka enzi hizo ila ikiwa kwenye viwango zaidi.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO hii leo kama ulikuwa hujui au sikiliza kazi za kwaya hiyo ili kujua uchunguzi wa GK uko sawa? , vinginevyo tukutane wiki ijayo...
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.