KWA TAARIFA YAKO: KWAYA TOKA KIJIJINI ILIVYOWEZA KUZIPIKU KWAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. KaribuKWA TAARIFA YAKO hii leo tupo huko mkoa mpya uliopatikana ndani ya mkoa wa Iringa zamani ilikuwa ikijulikana kama wilaya, nazungumzia mkoa wa Njombe ambao unasifika kwakuwa na baridi kali lakini pia kilimo cha chai na kinakubali sana. KWA TAARIFA YAKO leo hii nataka kuzungumza kuhusu kwaya moja iliyoweza kujitambulisha vyema kwenye medani ya muziki wa injili mwanzoni mwa miaka ya 90. Kwaya hii kwayeyote aliyepata kusikiliza album zake asingeweza kuamini kwamba inatokea huko Njombe.

KWA TAARIFA YAKO nazungumzia kwaya kutoka kanisa kuu la Anglikana mkoani Njombe iitwayo "Njombe Anglican Cathedral Choir"kwaya hii iliweza kutoa album mbili zilizopangiliwa vyema kuanzia uimbaji mpaka muziki, nachelea kusema kwayeyote aliyesikiliza miaka hiyo ya 93 au 94 kwaya hii iliimba kama kwaya inayotokea katikati ya jiji la Dar es salaam maana kanda zake zilikuwa na ubora kuliko hata baadhi ya kwaya zenyewe zilizokuwapo jijini Dar es salaam kwa wakati huo.KWA TAARIFA YAKO kanda iliyokuwa ya kwanza kutoka katika kwaya hii inaitwa "Sikilizeni" kuna nyimbo kama ninatamani, sikilizeni, Zakayo na nyingine lakini pia waliweka pambio moja la kibena ndani yake liitwalo 'Suke suke' ambalo kwa wakati huo likaja kuwa maarufu na kupigwa kwenye sherehe mbalimbali hususani harusi hasa wahusika wakiwa ni wenyeji wa mkoa wa Iringa. KWA TAARIFA YAKO kwaya hii ilikuwa kama kwaya namba mbili kujulikana katika kwaya za kanisa Anglikana wakitanguliwa na Tumaini 'Shangilieni' kwaya ya Arusha.

KWA TAARIFA YAKO kwaya hii iliamua kutoa kanda maalumu ya nyimbo ama mapambio ya kitamaduni ambayo pia naweza kuthubutu kwamba hawakukosea kwa maana ya ubora wake kuanzia upigaji hadi uimbaji kanda hiyo ilikuwa na nyimbo kama 'Vakwinoma' na mapambio mengineyo na kufanya wajulikane zaidi hasa ukizingatia miaka hiyo watu walianza kujitutumua kuachana na harusi za kufanyia majumbani kwa kuzungushia na makuti ya mnazi na kuanza kuhamia katika kumbi, ambazo kwa wakati huo zilikuwa kama Msimbazi Centre, uwanja wa ndani wa Taifa, PTA na nyinginezo huko kote nyimbo za kwaya hii zilikuwa zikipigwa sana.


Baadhi ya wanakwaya wa sasa wa kwaya hiyo wakiwa kwenye huduma Ludewa


KWA TAARIFA YAKO kwaya hii bado ipo ikingali ikiutangaza ukuu wa Mungu, pia imefanikiwa kutoa video ya nyimbo za 'Sikilizeni' lakini kikubwa zaidi ambacho nimeipendea kwaya hii, imefanya jambo ambalo hata kwa kwaya za mjini sio zote zilizokumbuka kufanya hivyo kwakufungua ukurasa wake wa Facebook ili kuwasiliana na wapendwa wao wanaofuatilia huduma yao, kuna kwaya zipo Dar es salaam na asilimia 90 za waimbaji wake wapo Facebook lakini wamesahau kuwa na mawasiliano ya namna hii ilikuisaidia huduma yao kufahamika kwa watu wengi zaidi.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo….

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.