KWETU PAZURI WAPO TAYARI NA DVD MPYA YA 11


Baada ya kuachia DVD yao ya 10 iitwayo 'Ibatebuli' ikiwa mchanganyiko wa nyimbo mpya na za zamani walizowahi kurekodi kwa lugha ya kwao na kiswahili lakini wakitafsiri kwa lugha ya bemba na Tonga za nchini Zambia. Kwaya maarufu katika ukanda wa Afrika mashariki na kati ya Ambassadors of Christ almaarufu kama 'Kwetu Pazuri' ya kanisa Sabato Remera jijini Kigali nchini Rwanda wanatarajia kuachia DVD mpya ya 11 mwezi April.

Kwa mujibu wa taarifa kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, kundi hilo limeweka baadhi ya picha kutoka katika DVD hiyo ambayo hata hivyo hawajaweka wazi kama zitakuwa nyimbo mpya walizoimba kwa lugha yao pekee ama wamechanganya na lugha ya Kiswahili. Aidha katika taarifa hiyo kundi hilo limeonyesha shukrani zao za dhati kwa Mungu kwa jinsi alivyowapitisha katika mitego ya shetani ambaye alidhani amewaweza lakini wakashinda na zaidi kuwataka watu kukaa tayari kutiwa moyo na kupata faraja kupitia nyimbo zenye ujumbe mzito zilizomo katika album hiyo.

Wakati huohuo wakati kundi hilo likiwa linatarajia kutoa DVD hiyo ya 11 tayari maandalizi ya toleo la 12 yanatarajiwa kuanza hivi karibuni na kuwataka waamini kuendelea kuombea kazi hiyo.


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.