MAMBO MACHACHE UNAYOWEZA KUFANYA AKILI YAKO INAPOCHOKA

Na Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

1. TAFUTA MUDA WA KUPUMZIKA/LIKIZO. 
Akili inapochoka, mwili mzima unashindwa kufanya kazi katika kiwango chake kinachopaswa kwenye maisha ya kila siku. Unapoilazimisha akili ifanye kazi kwa lazima ni kama kulazimisha mwili uliochoka ufanye kazi ngumu. Matatizo mengi tunayokutana nayo kwenye maisha ya kila siku muda mwingi yanasababishwa na akili zetu kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Hii inatokana na uchovu ambao akili yetu imekuwa ikiupata. Kufanya kazi nyingi zinazotumia akili kwa muda mrefu hupelekea Mwili kuchoka. Katika kila mwaka unapaswa kuwa na Siku 28 za kupumzika ili akili na mwili wako vikae sawa kwa ajili ya kuanza utendaji mpya. Lakini pia inakupasa kwa kila wiki uwe na siku moja ambayo utafanya mapumziko ya akili. Kitaalamu pia haupaswi kufanya kazi mfululizo zaidi ya dakika 45. Inapaswa kila baada ya dakika 45 ufanye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na kazi husika.

2. JITENGE MBALI KIDOGO NA WATU KWA MUDA FULANI. 
Iwapo utagundua akili imechoka na mara nyingi unaona shughuli zako zinahusisha na mijumuuiko ya watu. Jifunze kuwa na muda binafsi wa kupumzika kwa muda fulani. Muda wako binafsi utakusaidia kupumzisha akili yako kwa Kiasi fulani bila kuwa na muingiliano na watu wengi. Mara nyingi hata wenye familia hutumia muda fulani wa kufanya retreat kidogo kama mke na mume tu na kuwaacha watoto nyumbani. Kazi ya malezi ya watoto kwa muda mrefu huchosha akili na mwili ndio maana hushauriwa ili waendelee kuwa na kiwango kizuri cha malezi lazima wajipangie muda kidogo wa wao binafsi kuwa na mapumziko.Vile vile hata kama hauna familia, unapogundua akili imechoka/imezidiwa, jifunze kujitenga mbali na watu kidogo ili kuweza kupumzisha akili yako kwa muda fulani.

3. MAWASILIANO
Akili inapokuwa imechoka, ubora wa mawasiliano kati ya kwako na watu wengine hupungua. Kumbuka sio kila kuongea ni kuwasiliana. Unaweza ukaongea lakini haujawasiliana na watu wako uwapendao. Unapogundua akili imechoka/imezidiwa, punguza mawasiliano yasiyokuwa na ulazima. Unapokuwa na mawasiliano ya ulazima, mara nyingi unaendelea kuchosha akili yako pasipokuwa na ulazima. Iwapo wewe ni muongeaji, punguza kuongea maana wakati huu unaweza ukaongea chochote ukijua umewasiliana kumbe umeharibu. Iwapo unatumia mitandao ya kijamii punguza utumizi wake. Pia kama unaweza kuzima simu kwa muda fulani iwapo haina ulazima wa kuwa wazi fanya Vivyo. Iwapo utashindwa kufanya Vivyo tafuta namba ya simu mbadala ambayo unaweza kuwasiliana na watu wako wa karibu tu kwa Kipindi ambacho utahitaji kupumzika. Muingiliano usiokuwa na ulazima na mambo mengi hupelekea kuongeza uchovu wa akili na kupelekea akili kufanya kazi kwa ufanisi mdogo zaidi ya kawaida.

4. TAFUTA SHUGHULI MBADALA YA KUFANYA.
Iwapo wewe unafanya kazi ya taaluma fulani kwa muda mrefu na kupelekea akili yako kuchoka jaribu kutafuta shughuli mbadala ya kufanya badala ya taaluma ambayo umeisomiea au umekuwa ukifanya kazi kwa muda mrefu. Tumia Muda huu kujaribu kujishughulisha na michezo mbalimbali, mfano kuogelea, kucheza muziki, kuimba, na mengineyo kama hayo. Unaweza kutumia muda huu kusoma vitabu nje ya taaluma yako, mfano vitabu vya vichekesho, vitabu vya hadithi na nyingine mbalimbali ambazo unahisi zinaweza kusaidia kupumzisha akili yako na kuondoa uchovu uliomo kichwani. Ili kuondoa uchovu wa akili, haupaswi kutumia nguvu nyingi sababu badala ya kuipumzisha akili, utazidi kuichosha zaidi. Tafuta shughuli mbadala ambayo italeta burudiko jipya kwenye akili. Akili hupenda kujifunza mambo mapya. Akili inapofanya jambo moja kwa muda mrefu huchoka kwa haraka zaidi.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.