MASWALI MACHACHE YA KUJIULIZA PINDI UNAPOGUNDUA UPO KATIKA KILINDI CHA TATIZO

Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

©Passion Pride Purpose
 Hakuna Mtu ambaye hajawahi kukosea kwenye maisha ,wote tunakosea inategemea aina ya makosa tunayokosea kuna Makosa ya Kitaaluma, Makosa ya Kifamilia ,Makosa ya Kifedha,Makosa ya Kisiasa  na Mengineyo.Makosa yamegawanyika kwenye makundi mbali mbali na yako ya kila namna.Makosa haya ambayo tunayafanya hupelekea kuingia kwenye aina fulani ya Tatizo linaweza kuwa la Kiafya,Kifedha,Kisiasa,Kifamilia na Mengineyo

Maumivu mengi tulio nayo kwenye jamii leo  ni matokeo ya makosa mbali mbali ambayo yalifanyika hapo mwanzo huenda kwa kujua au kutokujua.Kosa lolote linapofanyika kwa namna moja au nyingine lazima kuna adhabu ina ambatana na kosa husika.Hakuna Kosa ambalo halina adhabu ,Inawezeka adhabu hiyo ikawa moja kwa moja au kwa namna nyingine.Maumivu ni moja ya Ishara Muhimu kwamba kuna jambo lazima lirekebishwe haraka ili ili Maimivu hayo yasirejee tena.Makosa tunayoyagundua ni ishara ya kwamba imetupasa kurekebisha jambo fulani ili tuweze kufikia kiwango cha Ukamilifu.
Yafwatayo ni Maswali Machache ambayo Unaweza Kujiuliza Pindi Unapogundua Umekosea na Umeingia kwenye Tatizo Husika.

1. Je ni Aina Gani ya Maamuzi Uliyoyafanya Mpaka Ukafikia Kuingia kwenye Tatizo Husika?

Muda Mwingi tunapokuwa tumepatwa na Maumivu yaitokana na aina fulani ya makosa maishani mwetu tumekuwa tukiangalia Maumivu yaliotupata bila Kugundua kwamba Maumivu ni Hitimisho tu lakini sio chanzo cha tatizo.Unapoona Umekosea jambo hakikisha unaanza kwa kujiuliza mpaka hapoa ulipofika kukosea ni Maamuzi gani uliyafanya kwenye kila hatua na Je Hizo hatua zilikua na maamuzi sahihi?Unapofwatilia kwa umakini utagundua kwenyehatua fulani kuna kosa ulifanya ndio maana kuna hilo tokeo?Epuka kuaanza kwa kulaumu mtu anza kwa kujiuliza wewe binafsi.Watu kuja au kutokuja kwenye maisha yako ni matokeo ya maamuzi yako na sio wao.Ili kupata Matokeo bora baadilisha mfumo wako wa Maamuzi kwenye maswala mbali mbali kuepusha makosa ambayo hayana tija.

2. Je Tatizo Lililotokea Linasabibishwa na Sababu za Ki-Imani?

Muda Mwingi tumekuwa wa kwanza kumlaumu Mungu au Shetani kwenye Mambo fulani yanayotupa na  tunapokua kwenye kilindi cha tatizo.Lakini kiukweli Unaweza kukuta asilimia 90% ya Maatizo yanayotukuta  ni kutokana na Maamuzi yetu mabaya hapo Nyuma.Yapo Matatizo  yanasababishwa na Ushawishi wa Ki-shetani lakini sio yote.Fwatilia kwa Kina kabla ya Kusema tatizo hili na la Ki-Imani.Tatizo la Ki-Imani hushughulikiwa Kiimani.Mfano Unaweza Kukuta Asilimi 50 ya Watoto Wanaumwa Vichaa,Tunaanza kusema Shetani Kumbe jamii husika Wanavuta Bangi.Takwimu Mpya Zilizotolewa na Tume Mbali Mbali za Utumizi wa Dawa za Kulevya Inaonyesha Kati ya Kila Vijana 50,25 wanatumia dawa za Kulevya yaani wastani wa Vijana 5 kati ya kila Vijana 10.Hili Sio tatizo la Ki-Imani  ni kuhakikisha elimu inatolewa na kuhakikisha Dawa husika haziingii nchini. Hakikisha Unajua Chanzo cha tatizo Katika Uhalisia wake kabla ya Kufikia hitimisho.

3. Je Ni Aina Gani Ya Ushauri Niliupokea  Kabla Kuingia kwenye  Tatizo?

Hakuna Mtu yeyote Duniani ambaye aliweza kuendelea aua kufikia kiwango kikubwa cha mafanikio bila kuwa na washauri.Washauri wanaweza wasie ki-ofisi  moja kwa moja lakini maneno yao juu ya maswala mbali mbali yanaathiri maamuzi yako kwenye maisha yako ya kila Siku.Ni Muhimu kuhakisha unakuwa na watu ambao wanakushauri kwa Umakini na wana-Upeo mkubwa kwenye hicho wanachkoshauri.
Ukiona tatizo limetokea kwenye jambo lolote huwa kuna mambo matatu ; Ushauri Uliopewa sio Sahihi,Haukupewa Ushauri Kabisa,Haukutendea Kazi Ushauri Uliopewa.Iwapo ulipewa Ushauri na Ukatendea kazi lakini Haukupata Matokeo Chanya Badilisha aina ya washauri wako,Iwapo Haukupata Ushauri tafuta Ushauri wa Kina na Iwapo Haukutendea kazi Ushauri Husika anza Kutendea kazi ili tatizo husika lisireje tena.

4. Je Lipi Ni Suluhisho la Haraka na la Kudumu Juu ya Tatizo Unalopitia?

Kosa lilisotafutiwa suluhisho la Haraka na La Kudumu mara nyingi huongeza Msongo wa Mawazo kwa Kiasi Kikubwa.Ni Muhimu kujua sulihisho haraka iwezekanavyo ili kupunguza Msongo wa Mawazo.Iwapo tatizo  hilo halina Sulihisho la Haraka na la Kudumu ni muhimu kusubiri ili kutokusababisha matatizo zaidi na zaidi kwenye Titizo moja ambalo limeshatokeo.Hakikisha Unatulia kwa Umakini na Tafakuru ya Kina  kabla ya kufanya Uamuzi wewote kwa haraka iwapo unaona Uamuzi huo utakuwa wa Muda na hautaleta tiba ya kudumu Tatizo husika lisijirudie tena na tena.

5. Je Angekuwa Mtu Mwingine Ningempa Ushauri  Gani  Juu ya Tatizo Husika?

Mara nyingi watu wanapopatwa na Matatizo,Hutujia na kutaka  ushauri.Mara nyingi huwa tunawapa ushauri mzuri ambao huwanasau kwenye matatizo  yao wanayopitia  lakini pale tunapobanwa   na matatizo tunashindwa kujishauri na huenda tukajikuta na tunafanya makosa zaidi na zaidi.Unapopatwa natatizo  Jiulize Swali hili kwamba Je angekuwa mtu mwingine ningempa Ushauri gani ambao utamnasua kwenye tatizo  Husika na Mara unaweza kuta unapata majibu ambayo haukuyataraji na yanaweza kukuvusha katika tatizo husika lisijitokeze tena.

Mwisho

Unapogundua umefanya tatizo  kwenye jambo fulani na kupelekea kupatwa maumivu ni muhimu kutulia sana kabla ya kwenda hatua nyingine.Hakikisha Unajiuliza maswali sahihi ambayo yatakuvusha hatua moja kwenda nyingine.Epuka kujiuliza maswali ambayo yatakufariji lakini hayakupi sulihisho la kudumu juu ya tatizo ambalo lilitokea na likapelekea maumivu.Jifunze kutofautisha Ukweli halisi(Actual Truth) na Ukweli wa Kufikirika( Perceived Truth) ili kuweza kupata suluhisho la Kudumu.Kuna Maswali Mengine ni kweli kabisa lakini Sio Halisi ni ya Kufikirika tu na hayakupi mwanga wa kuvuka na kukuwezesha kusonga mbele kwa kasi unayoitaka.Napenda Kumalizia kwa Kusema Usipende Tatizo Husika Jifunze Kuangalia Mwanzo wa Tatizo.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.