MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AWASIHI WAKRISTO KUSIMAMA KWENYE NAFASI ZAO

MKuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda pamoja na mkewe (kushoto kwake) wakisalimia kanisa baada ya kukaribishwa na Mchungaji Lilian Ndegi
Mkuu mpya wa Wilaya Kinondoni, Paul Makonda, amewasihi Wakristo kusimama katika nafasi zao ili kushughulika na mambo mbalimbali yanayotokea nchini. Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo alipokaribishwa kusalimia kwenye ibada kwenye kanisa la Living Water Centre Makuti Kawe, huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru Mungu kwa uteuzi huo wa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Paul Makonda aliongozana na kke wake katika Ibada hiyo, ambapo kanisa hilo linaloongozwa na mtumishi wa Mungu Apostle Ndegi ndio kanisa lililomlea tangu anasoma chuo, kabla ya kuingia kwenye siasa mpaka kupata uteuzi huo.

Katika salamu zake, Makonda ameeleza kumshukuru Mungu kwa nafasi ya uteuzi huo kwa kusema kwamba kwa namna Kinondoni inavyoongoza kuwa Wilaya kubwa na inayoongoza kwa miradi mbalimbali ya Kiserikali na mambo mengi ikiwemo mambo mabaya kama machangudoa, vibaka, madawa ya kulevya na uharibifu mwingi - ni Wakristo tunaoweza kusimama katika zamu zetu na kushughulika  na hali hizo, na hatimaye tukawa na wilaya yenye matukio yenye kumpa Mungu utukufu. alisema mkuu huyo wa wilaya.

Kufika kwa familia hiyo kanisani hapo hakukuwa bure, kwani Wakristo waliwafanyia maombi ili Mungu akapate kuwawezesha katika utumishi wao.


 Picha kwa hisani ya Idara ya Habari, Living Water Centre, DSM.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.