CHURCH BOY NA CHURCH GIRL YAZINDULIWA RASMI ARUSHA

Sehemu ya vijana waliofika siku hiyo katika picha ya pamoja.
Jumapili iliyoisha Jijini Arusha kumekuwa na amtukio kadha wa kadha, mojawapo likiwepo la kuzinduliwa kwa mradi wa Church Boy na Church Girl kwenye kanisa la EAGT Elerai linaloongozwa na Mchungaji Marko Haule. GK ambayo ilikuwepo kwenye tukio inakuletea picha za matukio zikiambatana na maelezo ya namna dhana nzima ya Church Boy na Church Girl ilivyotizamiwa.
Elder Tolla'g akimkaribisha Mchungaji Mbilla madhabahuni.
Pamoja na uzinduzi huo, mgeni rasmi, Mchungaji Lucas Mbilla kutoka aliwataka vijana kutodharau vitu ambavyo Mungu ameweka ndani ya maisha yao ama anavyosema juu yao kama ambavyo alifanya mke wa Ibrahim.Maelezo ya Mradi
Church Boy na Church Girl ni project inayodhamiria kumjengea mtazamo chanya kijana anayempenda Mungu na anaye tumika au anayetamani kutumika kwa kutumia mbinu za kipekee na za kisasa kufikia vijana wengi kwa habari njema ya Yesu Kristo.

Maneno mengi yanayosemwa miongoni mwa vijana kuhusu kuokoka ukiwa kijana na kuanza kumtumikia Mungu katika umri mdogo huwa si mazuri sana; wengi huona kuokoka ni “ushamba”, ”kupitwa na wakati”, ”kupoteza muda”, tena wengi tumeona mambo ya kanisa kuwa “so boring” hata hatutamani kujihusisha nayo.

Ni swali la kujiuliza kwanini vijana hata wale tulio makanisani tunakuwa so inspired and attracted to people ambao hawako makanisani. Labda tunakosea kuuliza ngoja tujaribu hivi… Kwanini watu wanaoinspire na kuattract vijana hawatokei makanisani? Tunajaribu kujenga picha ili uone kwa namna hii project ionavyo… What exactly the missing puzzle is?

Tunatamani kuona vijana wengi wakipata hamu ya kuishi maisha ya kikristo, tukitamani kumjua Mungu na kumtumikia. Zaidi vijana wa makanisani tuinuke na kuwa mifano kwa wengine, tukiwavutia wengine walio nje na kuwavuta kwa Yesu. Sisi tuwe msaada kwa vijana wengine, lakini pia kuweka daraja kati ya vijana na watu wazima kwa sababu tunawahitaji sana katika kukua kwetu.


MAONO
Ni kugeuza fikra za vijana na mitazamo tofauti waliyo nayo kuhusu wokovu.

DIRA
Ni kuanzisha kizazi cha vijana wenye uhusiano mzuri na Mungu

LENGO
Kuongeza idadi ya vijana kuwa na uelewa zaidi juu ya neno la Mungu na kutekeleza katika maisha yao ya kila siku.


MALENGO
· Kutoa mafunzo ya uchambuzi juu ya ukweli halisi wa maisha.

· Kufanya ubunifu mzuri kati ya vijana katika maeneo ya Tanzania. · Kuungana vijana na wadau wa maendeleo ili waweze kuletwa na ulimwengu wa uwezekano.


SHUGHULI 
Shughuli zetu ni kichocheo nguvu za kubadili mitizamo ya vijana

1. MAJADILIANO (Talk Shows): 
Tutaandaa majadiliano yenye kuhamasisha vijana kutafuta ufumbuzi bora wenye kuboresha maisha yao na kuwa makini na maisha.

2. MAZUNGUMZO: 
Kuleta pamoja vijana na wataalamu wengine kujadili changamoto na kutafuta kweli na mwisho ufumbuzi tena juu ya masuala yanayoathiri maendeleo ya vijana kufanya kazi katika mazingira ya kanisa.

3. MATAMASHA: 
Kuandaa matamasha ya kuishi ibada kwa kushirikiana na watu wengine kugawana maono sawa na sisi.

4. MAKALA YA VIDEO (Video Documentaries):
Kupitia makala yetu tunata kuiambia dunia kuwa Tanzania ina vijana ambao wako tayari kubadili Afrika, na mabadiliko ya njia ya ulimwengu anaona Afrika

MIKAKATI:Mpango huo umeunda mikakati ili kufikia maono na kuhakikisha uendelevu wake.

Baadhi ya mikakati ni:
· Makakati kiasi wa kipindi cha Majadiliano
· Mkakati wa uzalishaji video
· Mkakati wa usimamizi wa rasilimali watu

KUTOKA KWA GERALD BROWN KIONGOZI EFRAA MUSICA
Mmoja wa wana Church Girl, Victoria, baada ya kuelezea dhana ya mradi.

Elder Tolla'g
FDG DancersEfraa MusicaChurch Boy na nduguze
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.