MUULIZE VIA GK: BEATRICE MWAIPAJA AJA NA MAJIBU YAKO

Hujambo msomaji wetu wa Gospel Kitaa, karibu katika kipengele chetu cha "MUULIZE via GK" ambacho kinakujia kila siku za jumamosi ndani ya GK kinachokupa fursa ya kumuuliza msanii ama mtumishi yeyote wa Mungu swali moja kwa moja kupitia ukurasa wa Gospel Kitaa, na kwa kushirikiana na Gospel Celebration, utayapata majibu yako kwenye kipindi.

Leo Beatrice Mwaipaja ametufungulia pazia la msimu wa pili, na majibu ya maswali yako yote yapo hapa:


Frank Bundala Mutu Munene: Shaloom mpendwa,mimi namuliza Da Betrice kwamba kitu gani kilimpelekea kushawishika kufanya korabo na dada yake?
Like · Reply · 31 January at 12:46

Beatrice: Ya kwanza kabisa, kwanza mimi mwenyewe pia navutiwa na muziki wa dada yangu. Ni mmoja wa waimbaji ambaye ananibariki na mimi mwenyewe pia . Kwa hiyo pia nilipopata nafasi ya kufanya kazi na yeye ni dada alitoa wazo hilo, mdogo wangu tufanye album ya pamoja kwa hiyo nilifurahi sana, na nanikiukweli kufanya colabo na dada Martha mi namshukuru Mungu sana na nimefurahi sana.


Fatael Lyimo Prezdar Kutoka kinyerez dsm. Kwanza hongera kwa huduma. Naomba kujua tangu umeanza huduma yako ya uimbaji ni magum gani ambayo umekutana nayo na unaona ni changa moto kwako?
Na mbali na huduma hii ni kitu gani kingine unafanya? ni hayo tu Barkiwa.
Like · Reply · 31 January at 12:47

Beatrice:
Changamoto zipo lakini ndogondogo kwa upande wangu mimi changamoto niyolipata ni wakati wa kufanya video, video inahitaji pesa nyingi lakini pia video inahitaji maandalizi makubwa sana, kwa hiyo mambo yanaenda lakini kuna ugumu Fulani nakutana nao lakini namshukuru Mungu kuna watu wamenitangulia na wananisapoti vizuri, kwa hiyo namshukuru Mungu kwa hilo: sio magumu saana, lakini ni kama hayo.

Mbali na huduma kwa sasa hivi hakuna kitu nilichokifanya, isipokuwa nataka… yaani malengo yangu sasa nii… kwa sababu niko naandaa albam yangu ya pili, ambayo ntapontoa tu ntaelekea Kenya kwaajili ya kuongeza elimu namatani kusoma natamani kusoma tena kwa hiyo nna mpango kabisa wa kwenda Kenya kwa ajili ya kuendelea kusoma:Silva Thobias Napenda kufahamu yeye kama Msanii wa injili ambaye amekwisha kusikika au kama si kufahamika kwa wadau wa injili ana malengo gani kuwasaidia wasanii ambao wana malengo ya kumtumikia Mungu kwa uimbaji kama yeye?
Like · Reply · 31 January at 12:47

Beatrice:
Kwa sasa ninaweza kumsapoti mtu yeyote ambaye anahitaji msada kutoka kwangu, kwa uwezo ambao niko nao kidogo, ee mfano sasa hivi nimeshasapoti watu kama wawili, watatu, lakini kwa kuchangia kile kidogo yaani pale ambapo sehemu ambapo hawajaweza kupata kitu ambacho kikatosheleza kufanya kitu Fulani naweza kutoa huo mchongo wanitafute tu ntasaidia kwa sehemu ambayo Mungu na mimi atanipa nafasi ya kumsaidia.


Bari Yesu Shaloom mpendwa kunawasanii ambao wanapenda kumtumikia mungu kwanjia ya uwimbaji je? hawa mtawasaidiaje ili nawao wafanye uwinjilishaji.
Like · Reply · 31 January at 13:01

Beatrice: Mi naomba wanitafute kwa kiwango kidogo ambacho ninacho nitawasapoti.


Abby Jewel
Barikiwa beatrice kwa huduma, swali mbali na huduma ya uimbaji unajishuhulisha na nini? winnie cholela wa kibamba
Like · Reply · 31 January at 16:46

Beatrice: Hilo nimeshalitoa majibu

Jackson Nathan Ntungu
Kutoka tegeta dsm bwana asifiwe dada beatrice hongera sana kwa uimbaji mzuri swali langu ni changamoto gani unakutana nao wakati ulianza kuimba 2.ukiitwa mahali mfano mkutanoni kwenye tamasha unakuja au mpaka mshiko kwa ndio uende?3.ni mwimbaji gani unayempenda sana uimbaji wake la mwisho umeolewa? Barikiwa
Like · Reply · 1 February at 06:07


Beatrice:
Kwanza kabisa mi naweza, naimba sehemu yeyote, hata kama hawana kipato, chochote cha kunipa, ila tu waniambie ukweli kwamba Mwanetu njoo ntafika hapo lakini pia mwimbaji gani nampenda mimi (hahaa), nawapenda waimbaji wote lakini Nampenda zaidi, yaani naguswa zaidi na Bahati Bukuku, ninampenda sana kiukweli, alafu kuolewa bado, kuolewa bado, pia mimi ni mdogomdogo, bado sijaolewa. Changamoto nilizokutana nazo hasa ni upande wa studio, kwa sababau studio niliyofanyia mimi ni studio kubwa sana unaweza ukaenda ukakuta tayari watu wapo hivyo lakini nafikiri ni ndogondogo lakini nilikutana na changamoto nyingi;


Thobias Mayala
from kigambon je ni muimbaji gani wa gospel anayempenda?kwa sababu zp,anampenda?
Like · Reply · 1 February at 22:41

Beatrice:
(Mh haaa) Kwanza naweza kusema kwamba Waimbaji wote nawapenda lakini Bahati Bukuku ananivutia zaidi, hata maisha yake ambayo anaishi na watu, ni mwimbaji ambaye nipo karibu nae na ananishauri na pia nimemwona jinsi ambavyo anaishi na watu, nampende sana napenda uandikaji wake wa mistari yake, ni ukweli ni dada ambae amejishusha sana na Mungu amemwinua sana kwa hiyo nampenda sana hata nyimbo zake pia yaani nampenda sana.


Emmanuel Ezekiel Ezekiel Naitwa Emanuel Ezekiel! Mkurugenzi wa COME AND SEE PROMOTERS, Nampongeza Bitrice kwa kujituma na kufanya vizuri ktk muziki wa injili Tanzani.Swali langu ni muimbaji gan wa muziki wa injili anampenda na anatamani kufuanya nyayo zake na kufika alipo fika? Mwana Nzambe Mbepela Daniel Joseph Mnyamale Emmanuel Gripa
Like · Reply · 2 February at 12:45 · Edited

Beatrice:
Mimi nampenda Bahati Bukuku, Bahati Bukuku
Silas Mbise: Kwa hiyo nani ambaye ungependa kufuata nyayo zake
Beatrice: Bahati Bukuku

Margareth Benedictor Ndaluhekeye ubarikiwe dada kwa huduma yako je unamalengo gani juu ya huduma yako
Like · Reply · 4 February at 15:06

Beatrice:
Kiukweli nina malengo ya kufika mbali, lakini pia natamani sana kuimba live, kwa hivyo Mungu akinibariki kipato changu, Mungu atanisaidi nikapata vifaa vyote ambavyo vitaniwezehsa kuimba live natamani sana kuimba live.


Fred Kiguso mm naitwa fred john niko kibamba,swali langu kwa beatrice,nichangamoto gani anazokutana nazo katika huduma yake ya uimbaji?
Like · Reply · 1 · 31 January at 13:10

Beatrice:
Changamoto zipo lakini tumashukuru Mungu anatusaidia, ni changamoto ambazo tunakutana nazo zipo sehemu pia tunafika kufanya huduma lakini ukifika kule pia tofauti na makubaliano yaani changamoto ni nyingi sana kiukweli, zipo.

Silas Mbise: kwa niaba ya Ambwene Mwamwaja na Elie John ambao ndo tunakamilisha timu nzima ya Gospel Kitaa nikushukuru sana Beatrice Mwaipaja.

Beatrice: Amina, ahsante sana nashukuru.

Silas Mbise: Umefanya kolabo wewe na dada yako Martha Mwaipaja, vipi mpaka sasa hivi mmefikia wapi naona kimya.

Beatrice: Sasa hivi ndio tupo tunamlaizia video ya hiyo albam, na tulikuwa tunampango itoka hivi karibuni, lakini tumeona tutoa mwezi wa tatu mwishoni itakuwa imetoka tumeachia video, lakini audio ipo sokoni.

Silas Mbise: Beatrice Mwaipaja kuna mawasiliano yoyote ambayo msikilizaji anaweza kuyapata na pia mfuatiliaji na msomaji wa Gospel Kitaa?

Beatrice Mwaipaja: ndio, namba yangu 0654345737

Silas Mbise: Facebook tunaweza kukupata?

Beatrice: Facebook mtanipata pia
Silas Mbise: Jina gani?
Beatrice: Beatrice Mwaipaja

Pata kionjo cha wimbo wa Safari.

Wiki ijayo tutakuwa na muimbaji kutoka jijini Arusha, Engineer Carlos Mkundi. Pamoja na uimbaji, yeye pia ni Mkurugenzi wa Mkundi Promotions, waandaaji wa matamasha ya Onyesha Upendo kwa Mama. tutumie swali lako kwa barua pepe, lakini pia kupitia ukurasa wetu wa facebook.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.