MUULIZE VIA GK: ENGINEER CARLOS MKUNDI AJIBU MASWALI YAKO

Hujambo msomaji wetu wa Gospel Kitaa, karibu katika kipengele chetu cha "MUULIZE via GK" ambacho kinakujia kila siku za jumamosi ndani ya GK kinachokupa fursa ya kumuuliza msanii ama mtumishi yeyote wa Mungu swali moja kwa moja kupitia ukurasa wa Gospel Kitaa, na kwa kushirikiana na Gospel Celebration, utayapata majibu yako kwenye kipindi.

Hatimaye Engineer Carlos Mkundi amejibu kila swali ambalo lilihitaji ufafanuzi kutoka kwako. majibu yote yako hapa.


Sikiliza sauti yake, na pia unaweza kuipakua kwa kubofya hapa

Silva Thobias Shalom Mtumishi! napenda kufahamu kutoka kwake ni kipi kilichomsukuma mpaka kuanzisha matamasha ya Onesha Upenda kwa Mama?
Like · Reply · 7 February at 14:58

Engineer Carlos Mkundi: Shalom, ndiondio ninashukuru sana ee kwa hilo swali na pia kuwa mfuatiliaji wa matamasha yetu kwa upendo kwa mama; kitu kikubwa basi nini kilinisukuma au kuanzisha ni kutokana na ukweli uliwepo kabisa kwenye jamii, yaani kubwa au maendeleo makubwa ya nchi ambazo zimeendelea zinatokana na kuwapa uthamani wanawake au kuwapa uthamani hawa mama ambao watuleta dunia na pia halipingiki kwamba uwepo wetu sisi au mimi ninapokuuliza swali mtangazaji hapa ukisikiliza uwepo wetu sisi umetokana na mama kwa hiyo kabisa unaweza kuona kwamba mama ni mtu ambaye ana umuhimu kwenye jamii au ananafasi kubwa kwenye jamii lakini bado haijawa wazi kwamba huyu mama kweli ni wa muhimu, nchi kama ya Rasia ambayo, nchi kama uingereza ni nchi ambazo zimetambua umuhimu wa mama na umewapa nafasi, lakini hapo asilimia 89 au asilimi 90 ya watu ambao wanaongoza kule kama madiractor au kama wakuu wa idara tofauti tofauti kule urusi ni wanawake kwa hiyo unaweza kuona kwamba ni nchi ambayo ina maendeleo lakini wanawake wanafanya na hiyo nchi inaweza kuwa na maendeleo makubwa zaidi, kwa hivyo baada ya nilivyoona hivyo umuhimu wa hawa kina mama nikaona nianzishe au nitoke kwa msukumo mkubwa ambao Mungu amenipa nitoke na niweze kufanya haya matamanasha na lengo kubwa la haya matamasha ni kuingia vijijini kuingia mahali popote ambapo kina mama wanakuwepo wana shidi nyingi tofautix2 tunasaidia nao kwa njia tofauti, wengine pia wanafamilia lakini waume zao wamekufa au wameachana na waume tunawasaidi kwa hali ambao wanakutana kama ni tatizo kabisa tunawasidia mtaji kuweza kufikia malengo kwa hiyo kikubwa nilichokianzisha hiki kinatokana pia na uthamini wa hawa kina mama na hawa kina mama tukiwaelimiesha au tukiwasaidia wanaweza kufanya kitu kikubwa katika nchi. 

Fred Kiguso fred john kutoka kibamba, shaloom mimi nataka kujua kutoka kwa mtumishi ,nini malengo ya matamasha hayo ya onesha upendo kwa mama?
Like · Reply · 7 February at 21:29


Engineer Carlos Mkundi: Nashukuru sana, kutoka kibamba, lengo la matamasha haya ni kuonyesha uthamani wa mama lakini pia kuweza kujua umuhimu wa kina mama kwenye jamii kuwapa umuhimi wao lakini pia kuwasaidia kina mama kimtaji kihali yoyote ambao inawezekana kufanya nao kazi kwaukaribu zaidi yaani sio wao kuoneneka ni watu wa wakaida au ni watu wa kupita nyumbani lakini ni watu ambao wanaweza kufanya mambo makubwa katika nchi. 

Dotto DK Wa kigamboni DSM
SWALI: Engineer nijina tu lakupewa nawazazi au professional yako?
pia naomba historia yako kifupi mpaka ulipo sasa!
GC&GK PAMOJA ZAIDI
Like · Reply · 8 February at 16:13


Engineer Carlos Mkundi: Hii ni profession yangu bwana, engineer sio jina ni profession yangu, ambao mimi ni mechanical enginner. Kwa watu ambao wanaajiri na kuna magari ya yanahusika na utaliii Arusha au Tanzania au Afrika haya magari mimi ndio nimesomea mimi ni mechanical kwa hiyo nimezidi zaidi kwenye body building ambayo tunatengeneza magari ya utalii kwa ajili ya kwenda porini, kwaajili ya kupokea wageni hiyo ndio profession yangu kabisa.

Aha kwa kifupi mimi nilizaliwa Arusha, lakini baada ya kuzaliwa Arusha nilitokaaa ndani ya mwaka mmoja tu, nikarudi Dar kwa hiyo nikasoma kule Dar es Salam nikasoma Mbagala Kuu nikatoka Mbagala Kuu kuu nikawa naishi pale Mbagala Kizuiani, nikatoka hapo nikawa naishi Yombo Vituka, nikatoka hapo Vituka nikasoma Azania Secondary pale karibu na Jangwani baada ya hapo ndio nikaendelea na maisha mengine ya chuo nje ya nchi.


Fatael Lyimo Prezdar Kutoka kinyerez. Mbali na huduma yako ya uaandaaji wa matamasha ya upendo kwa mama', Ni neno gani au mstari gani unaosimamia ktk huduma yako ya uimbaji.??
Like · Reply · 1 · 7 February at 13:51


Engineer Carlos Mkundi: Eee, mstari mkubwa ambao mimi nautumia au naoupenda nii Yohana 5:1 unaweza kuona pale nuru ilingaa gizani wala giza halikuiweza; maana ya hii kubwa ni kwamba ufahamu unapoingia katika nchi au watu wanapokuwa katika ufahamu wa vitu vingi vingi ni rahisi watu kujikwamua na kufanya vitu vingi sana yaani watu wanakuwa hawapo gizani mfano kama leo ni siku ya valentine, lakin watu wanavyaofanya ni tofauti na vile Marekani wanavyofanya lakini tu ni ufahamu haupo kwa sababu tu ni ufahamu haupo ufahamu lakin watu wangekuwa na ufahamu hiyo ni nuru wangeza kufanya mambo makubwa zaidi.


Silas Mbise: Engineer Carlos nikushukuru sana kwa muda wako, kwa niaba ya timu nzima ya Gospel Kitaa, ambayo yuko Elie John ambaye yuko Arusha, na Ambwene Mwamwaja ambaye yuko Uingereza. Lakini nina swali tena kidogo kwako,  unaandaa matamasha ya Upendo kwa Mama, na mwaka huu pia umefanya jijini Dar es Salaam, je una mpango gani tena kuhusiana na matamasha ya Upendo kwa Mama?


Engineer Carlos Mkundi: Aah mpango ni mkubwa sana, kwa sasahivi kwasababu haya matamasha watu wameyapokea kwenye perfomance kubwa nchini, sio nchini tu nje ya nchi. Kwahiyo unaweza kuona ni kitu ambacho kinahitaji gharama kubwa lakini pia watu wenye uhitaji ni wengi sana.

Kwahiyo nilikaa chini na kugundua kwamba mbinu nyingine ya kuhakikisha tunawafikia watu wenye uhitaji kwasababu tunapigiwa simu kutoka mikoa tofauti tofauti wanafikiwa na funds au zile uzalishaji wa hizo pesa zinapatikana wapi licha ya kwamba mimi mwenyewe ninachangia kwa asilimia 100 hadi sasa hivi ni jinsi gani unaweza kujikwamua. Kwahiyo tutapata namba ya ambayo tutakuwa tunatengeneza mashindano, kwahiyo tutakuwa na watu ambao wanaimba nyimbo za mama na wanapigiwa kura, wakati huohuo wananchi watakuwa wananchangia kutokana na kupigia kura lakini pia kuwapendekeza wale watu waweze kushinda. Lakini pia wamama wote ambao watakuwa na mahitaji, watakuwa wanarekodiwa wanaongea zile sauti na watu wanawapigia kura kuweza kufikia mama gani asaidiwe kwa haraka zaidi. Kwahiyo mpango ambao tumejipanga ni mkubwa ambao tunaenda kufanya nchi nzima lakini tunafanya pia kwa nguvu kubwa ili atleast hiyo impact na hilo lengo liweze kufika na ujumbe uweze kufika na mabadiliko yawepo.

Mimi nakuambia ukweli ndugu mtangazaji, kama watu watakubali kuamini kwamba mwanamke au mama ana uwezo wa kufanya kitu, wakikubali hilo ni rahisi zaidi kuweza kufanya kitu. Kwasababu ukiangalia nchi yetu sahivi wanasema ni nchi ya tatu kwa umaskini. Ni kwa sababu kuna mfumo ambao tunauendesha mara nyingi sana tumekuwa tukitumika kama mwanaume kufanya kazi peke yake au kuchukua majukumu ya kila kitu pasipo kuwashirikisha na hawa wengine. Lakini tukianza sasa utofauti kwamba tuwashirikishe na sisi tufanye, kwahiyo tutakuwa na nguvu mbili ambazo zitasaidiana kuweza kufikia malengo. Lakini pia kwa upande wa wanawake, wana udhaifu ambao hawaujui na ndo elimu ambayo tumeamua kuitoa kwa wanawake kabisa. Kwasababu unaposema wewe ni msaidizi, msaidizi automatically unatakiwa kuwa na nguvu mfano ni sawasawa na gari ambalo limekwama mahali na linahitajika kusukumwa msaidizi anayekuja kusukuma hilo gari lazima awena nguvu ku-push ili liweze kwenda, lakini sio mwanamke tu wewe ukiitwa msaidizi ni kukaa na kusubiri tu, we kazi yako kupika, kukaa na kusubiri au kutoa lawama tu, mwanaume wangu hafai mwanaume wangu hivi hapana, unatakiwa kusimama na wewe uweze kufanya uongeze nguvu extra, ndio maana ya msaidizi.

Silas Mbise: Nikushukuru sana Engineer Carlos, je kuna mawasiliano yoyote msikilizaji anaweza kupata kutoka kwako?

Engineer Carlos Mkundi: 0755400200, 0756400200 au ukurasa wangu wa facebook Upendo kwa Mamaau kama ni akaunti ya Mkundi facebook atapata au anaweza kuandika tu ONYESHA kwenda 15522 anaweza kuwasiliana na sisi.

Silas Mbise: Nikushukuru sana pia nikutakie mafanikio mema na kazi njema.

Engineer Carlos Mkundi: Amina

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.