PICHA 120+ MVUA YA BARAKA ILIVYOZINDULIWA JIJINI ARUSHA

Mtoto Miriam Paul na mgeni rasmi, Mchungaji Philemon Mollel.
Jumapili tuliyoiacha imekuwa na udhihirisho wa Mungu, hasa pale umati ulipojitokeza kwenye uzinduzi wa albamu ya Mtoto Miriam Paul jijini Arusha, kwenye Kanisa Katoliki Parokia ya Kijenge, ambapo waimbaji kadha wa kadha walijitokeza sanjari na waungaji mkono wa huduma yake. Sanjari nao, wnafunzi wenzake kutoka Upendo Friends School hawakukosekana wakiambatana na walimu wao.

Mvua ya Baraka, album ya Mtoto Miriam, inadhihirisha kwamba Mungu anatumia watu wake apendavyo, kwani licha ya kuelekea kuwa na umri wa miaka kumi, bado utoto haujarusisha nyuma kasi ya kumtumikia Mungu. Miriam amezaliwa tarehe 17 Machi 2005. Wewe umezaliwa lini na unamfanyia Mungu nini?

GK ilipiga kambi siko hiyo na hatimaye inakuletea matukio katika picha kama ambavyo iliyanasa, ambapo pamoja na kuchangia huduma hiyo, mgeni rasmi, Mchungaji Philemon Mollel, alipngoza kipindi cha maombi kwa dakika chache zilizokuwepo, na hatimaye mioyo ya watu kufunguliwa na kuwekwa huru.

Mabibi na Mwabwana, sasa namleta kwenu Mtoto Miriam Paul...

Wasaa wa risala
Muda wa maombi, nafasi hii muhimu haikukosekanaKisha Mvua ya Baraka ikazinduliwa rasmi na ahadi pamoja na machangizo kufanyika
Kisha kila mtu akashiriki baraka
Bahati sikiza, hizi ni milioni 5. Ghafla akatokea "Yesu"Wanafunzi wenzake kutoka Upendo Friends School walikuwepo kuonyesha upendo kwa mwenzao
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.