SAA 24 ZINATOSHA KULETA MABADILIKO KWENYE MAISHA YAKO

Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor
©The Todd & Erin Fav 5
Mara nyingi maisha ni muendelezo wa mabadiliko ya kila siku. Usipokuwa na mabadiliko kila siku maana yake hauna tofauti na jana wala hutokuwa na tofauti na juzi iwapo haukujifunza jambo lolote jipya.

Mara nyingi tumehisi kwamba tunahitaji muda mwingi na miaka mingi sana kuweza kubadilisha maisha yetu kwenye nyanja mbalimbali yaani  kiuchumi, kitaaluma, kijamii na kisiasa lakini ukweli wa mambo ni kwamba tunahitaji saa 24 tu kubadili maisha yetu. Jana ni siku ambayo imepita. Leo ndio siku ambayo tunayo na kesho hakuna ajuaye lipi linaweza kutupata zaidi ya Mungu ambaye ndio hupanga na kuamua matukio na mambo mbali mbali katika maisha yetu.

Je unafikiri ni kitu gani unapaswa kufanya ndani ya Saa 24? Saa ambazo ni sawa na Siku Moja ili kubadilisha naisha yako? Je umejaribu mara ngapi na bado haujaweza kufanikiwa kuleta mabadiliko ambayo unayatamani kwenye maisha yako? Yafwatayo ni Mambo ambayo yanaweza kukusaidia kubadili maisha yako ndani ya Saa 24.

1. Hakikisha Unachotaka Kubadilisha kwenye Maisha yako.

Kabla haujaamua kufanya badiliko lolote kwenye maisha yako hakikisha unajua na kukitambua kile unachotaka kukibadilisha kwa kufanya uchunguzi na upembuzi wa kina pia ikiwezekana hakikisha unakuwa na details za kutosha kabla ya kufanya badiliko lolote.Ni ngumu kujua unakotaka kwenda kama hauna ramani na maelezo ya kutosha.Ni muhimu sana kuhakikisha unakuwa na maelezo ya kutosha kabla ya kuchukua hatua ili kujua faida na hasara ya kile unachotaka kubadilisha kwenye maisha yako.

2. Hakikisha Kila Siku Unatenga Kati ya Dakika 30-45.

Ili kuweza kuwa mtalaamu wa jambo lolote au kupata Ujuzi wa kutosha kwenye jambo lolote Unahitaji Saa 20 tu kufikia kiwango cha Juu au kukaribia kiwango cha juu cha lengo lako.Unapo tumia kati ya 30-45 kwa Siku ndani ya Mwezi Mzima utakuwa umetumia Saa 20 ambazo zinaweza kuwa zimekupa ujuzi na mafaniko unayoyatarajia.Hakuna jambo ambalo lilianza kubwa kama unavyoliona leo.Jifunze kufanya kidogo kidogo.Kesho hatunayo lakini leo ndio yetu.Hakikisha unaitumia leo kwa Ukamilifu wake,Jana imeshapita.

3. Hakikisha Unakuwa na Mwelekeo Thabiti.

Kitu chochote ambacho kinaweza kukuvurugia ratiba yako ya Dakika 30-45 kwa Siku ni kwamba kinaweza kukuharibia kuweza kufikia lengo lako kubwa.Mwelekeo thabiti ni jambo la muhimu sana kwenye kile unachotaka kubadilisha kwenye maisha yako.Hakikisha unatumia muda wako Muhimu vizuri san asana ili kuweza kufikia lengo lako ambalo linpaswa kufikia saa 20 kwa Mwezi mzima bila kukatishwa katishwa njiani.Mwelekeo thabiti utakusaidia kupata matokeo unayoyahitaji kwa haraka kuliko ilivyo kawaida.

4. Hakikisha Unafanya Tathmini Kila Siku.

Tathmini ya kila siku itakusaidia kujua iwapo unasonga mbele au unarudi nyuma.Namna sahihi ya kufanya tathmini ya kila siku hakikisha unajenga tabia ya kuandika kila jambo ambalo unalofanya siku hiyo,Iwapo ni Matumizi yako ya Fedha,Iwapo Ni Mizunguko yako ya Siku,Ili unapofika wakati wa tathmini usipate tatizo la kuujiliza uliza au kupoteza muda sababu tayari taarifa za utendaji wako wa siku unazo na itakusaidi kujua kipi kiongezwe au kipi kipunguzwe ,kipi kifanyike na kipi kisifanyike.Ni Muhimu sana Sana,Ili uweze kuleta mabadiliko unayoyatarajia kwa muda mfupi yaani ndani ya saa 24 tu,unaweza ukawa umepata mabadiliko unayoyapata.

Hitimisho.

Unaweza  kufanya mabadiliko makubwa wakati mabadiliko madogo yanakushinda,Unawezaje kucheza mpira dakika tisini wakati hata kucheza dakika kumi ni tatizo.Huwezi kuleta mabadiliko makubwa wakati haya madogo madogo yankushinda.Mafanikio makubwa unayoyaona leo ni Mkusanyiko wa  Mafanikio Madogo Madogo ya kila siku na utendaji mdogo mdogo wa kila Siku.Unapoendelea mwaka 2015 hakikisha Neno "HALIWEZEKANI" linaondoka kwenye kamusi ya Misamiati yako kwa kubadilisha utendaji wako Mdogo Mdogo wa Kila Siku.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.