SOMO: KILA MTU ANA WAKATI WAKE WA VITA

©Pix Good

SOMO: KILA MTU ANA WAKATI WAKE WA VITA...
Ayubu 7:1
Je! Mtu hana wakati wake wa vita juu ya nchi? Na siku zake, je! Si kama siku za mwajiriwa?


Wakati wa vita sio wakatii wa wa faraha au kupumzika, ni wakati kupigana. Kila mtu ana wakati wake wa vita. Kila mtu anatakiwa ashinde vita yake, Vita ina mambo mawili, kushinda au kushindwa. Vita huwa ina gharama yake, na vita hufanya wengine wanapoteza katika maisha yao, unapoteza haki zao za msingi.

Ayubu 14:14
Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za vita vyangu, Hata kufunguliwa kwangu kunifikilie.

Mhubiri 3:8
Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.

Zaburi 3:6
Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.

Kwa vile dunia inavyoongozwa na uovu ndio maana kuna vita, vita ikitokea usianze kushangaa, anza kupigana, maana vita hua vinazuka tu, hata mbunguni vita ilianza tu. Kama hauko kwenye Amani au faraha ujue ni wakati wa vita, na kila vita ina gharama.

Kwenye eneo lenye Baraka zako vita inaelekezwa hapo, wewe ni askari lazima uende vitani. Unachokitaka kipo isipokuwa kuna vita. Vita yaweza kusababishwa lakini tunapigana lengo ni moja tu kushinda. Wakati wa vita sio wakati wa kutiwa moyo au kubembelezwa. Wala sio wakati wa kulaumiana, au kuongea sana, ni wakati wa kupambana.

Mithal 3:29
Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.

Efeso 6:10-12
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Huwezi kutiisha bila kupigana vita, huwezi kumiliki, wala kutawala bila kupigana vita. Vita hutokea bila taarifa, hivyo usipojua la kutenda unaweza kupoteza Vita ikitokea wewe anza kupigana, katikati ya vita Mungu anajitukuza, wakati wote kaa kivita vita. Ukishinda vita unapanda ngazi, hatua nyingine, kwa kadiri unashinda vita ndivyo unavyopanda.

Mithali 3:25
Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.


NA MCHUNGAJI KIONGOZI ISAYA KILYINGA
UFUFUO NA UZIMA- KILOMBERO

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.