SOMO: MUNGU KATIKA UZAO WA WANADAMU - MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA

Askofu mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima

SOMO: MUNGU KATIKA UZAO WA WANADAMU

Kuna mambo ambayo mkono wa polisi na jeshi hauwezi kufika lakini mkono wa Mungu unaweza kupafikia na kupagusa.

Kutoka 15:3 “Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.”
Panapofika wakati wa vita anakuwa mtu na Jehova ndilo jina lake, Panapofika wakati wa uongo hawi mtu anakuwa Bwana.

Mwanzo 1: 26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.”

Sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu. Mambo yote ambayo Roho mtakatifu anaweza kuyafanya na mimi naweza kuyafanya sababu nimeumbwa kwa mfano wa Mungu.

Mwanzo5: 3 “Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi.”
Kitu kinapozaliwa kwa sura na mfano huwa sawasawa na aliyekizaa, Seti aliweza kufanya kile ambacho Adamu alikifanya. Na sisi tunaweza kufanya kile ambacho Mungu alikifanya sababu sisi ni mfano wake.

Mwanzo18: 1 “Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona, na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, akasema, Bwana wangu, kama nimeona fadhili machoni pako nakuomba usinipite sasa mimi mtumwa wako. Na yaletwe basi maji kidogo mkanawe miguu, mkapumzike chini ya mti huu. Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, iwapo mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema. Basi Ibrahimu akaenda hima hemani kwa Sara, akasema, Himiza vipimo vitatu vya unga safi, uukande, ufanye mikate. Ibrahimu akapiga mbio kwenda kundini, akaleta ndama wa ng'ombe aliye laini, mzuri, akampa mtumishi, naye akahimiza kuiandaa. Akatwaa siagi na maziwa, na ndama aliyoiandaa, akawaandikia mbele yao, akasimama karibu nao chini ya mti, nao wakala”

Unapopanga vita unatakiwa ujue kwamba wakati wa vita Bwana ni mtu wa vita. Malaika huwa hawataki kuabudiwa sababu wao ni wajoli wetu, Mungu pekee ndiye astahilie kusujudiwa.

Ufunuo19: 1 “Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; wokovu na utukufu na nguvu zina BWANA MUNGU wetu. kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake. Wakasema mara ya pili, Haleluya. Na moshi wake hupaa juu hata milele na milele. Na wale wazee ishirini na wanne, na wale wenye uhai wanne, wakasujudu na kumwabudu Mungu, aketiye katika kile kiti cha enzi, wakisema, Amina, Haleluya. Sauti ikatoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Msifuni Mungu wetu, enyi watumwa wake wote, ninyi mnaomcha, wadogo kwa wakuu. Nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, na kama sauti ya maji mengi, na kama sauti ya radi yenye nguvu, ikisema, Haleluya; kwa kuwa Bwana Mungu wetu, Mwenyezi, amemiliki. Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing'arayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu. Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.”

Ufunuo 22: 1 “Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-Kondoo, katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.”

Yoshua 5: 13 “Ikawa hapo Yoshua alipokuwa karibu na mji wa Yeriko, akavua macho yake na kuangalia, na tazama, mtu mume akasimama kumkabili mbele yake, naye alikuwa na upanga wazi mkononi mwake; Yoshua akamwendea, na kumwambia, Je! Wewe u upande wetu, au upande wa adui zetu? Akasema, La, lakini nimekuja sasa, nili amiri wa jeshi la Bwana. Yoshua akapomoka kiusouso hata nchi, naye akasujudu, akamwuliza, Bwana wangu aniambia nini mimi mtumishi wake? Huyo amiri wa jeshi la Bwana akamwambia Yoshua, Vua viatu vyako miguuni mwako; kwa kuwa mahali hapo usimamapo ni patakatifu. Yoshua akafanya vivyo.

Yehova anao upanga wake ambao hauko halani mwake bali uko tayari kutenda kazi.
Yesu hatarudi kulinyakua kanisa mpaka baadhi ya mambo yafanyike hapa duniani.
Matendo ya mitume 3: 20 “Apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani; ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.”
Kuna nyakati zinakuja baadhi ya mambo yatafanywa upya, Yesu atabaki mbinguni mpaka mambo yote yafanywe upya.
Haya maneno yalisemwa na mtume Paulo kwenye karne ya kwanza, kanisa lilipoanza lilianza kama mwanakondoo yaani watu wa duniani walikuwa wanawaita wakristo kuwa ni mbwa mwitu na Yesu kristo aliitwa mwanakondoo, ndiomaana watu wa Mungu waliuwawa ‘mtume Petro alisulubishwa kichwa chini miguu juu, Tomaso alipigwa mishale ugiriki mpaka akafa, Mathayo aliburuzwa kwenye gari mpaka akafa, Bathlomeo alichunwa ngozi yake akawekwa kwenye mafuta yaliyochemka mpaka akafa, mashetani wakazoea kuuwa wakristo wengi wakijua yakwamba wakristo ni wapole, ni wa kupigwa shavu moja na kugeuza lingine lakini na sasa wakati umefika wa mambo hayo kufanywa upya mfano mambo ya kutishia

“Kwa jina la Yesu ninakataa kutishwa, ninavaa moyo wa ujasiri, moyo wa ushujaa kwa jina la Yesu.”

Mithali 4: 10 “Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako. Usiingie katika njia ya waovu, Wala usitembee katika njia ya wabaya. Jiepushe nayo, usipite karibu nayo, Igeukie mbali, ukaende zako. Maana hawalali isipokuwa wametenda madhara; Huondolewa usingizi, ikiwa hawakumwangusha mtu.”

Mtu anaweza kutumika na shetani kumtisha mtu/watu au kuharibu maisha ya mtu/watu kwa ngazi ya taifa au kifamilia au maisha binafsi, Mtu huyo anaweza kuwa yeye ni wakala wa kuzimu amekuja kutisha maisha yako, kuna wanaoishi maisha ya hofu kwasababu kuna watu wanaowataabisha ambao wameingia kwenye ustawi wa maisha yao.

“Hakuna maisha mazuri unayoweza kuyaishi isipokuwa umepewa na Mungu, hakuna mtu anayeweza kukatisha maisha yako na ile miaka uliyopewa na Mungu lazima itimie kwa jina la Yesu”.

“Kuna watu wanaagenda ya kulitisha taifa na kuna watu wanaagenda ya kukutisha maisha yako wao wanapenda wakuone unalia.”

“Kila aliyesimama katika uso wa dunia aliye na agenda ya siri mwenye lengo baya na kazi yako, maisha yako, furaha yako niwaapisha kwa jina la Yesu ninalivunja lile jambo lao la siri walilolipanga juu yako na familia yako kwa jina la Yesu kristo.”

Shambulia wale wote waliopanga mabaya na mashambulizi juu yako na Taifa shambulia na mahali wanapopatia nguvu zao kwa jina la Yesu.…
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.