TAMKO LA MCHUNGAJI GWAJIMA JUU YA VITISHO VYA KIGAIDI

Askofu Josephat Gwajima
Kwa siku kadhaa wananchi wamekuwa kwenye sintofahamu kutokana na jumbe video kadhaa ambazo zimeenea mtandaoni, kuhusu watu wanaojisifia kushambulia na kuua askari polisi. Kufuatia hilo Mchungaji Kiongozi wa kanisa la 'Ufufuo na Uzima', Askofu Josephat Gwajima, ametoa tamko kali kuhusiana na watu hao, naye akiwatia moyo viongozi wa taifa pamoja na wanausalama.

Sauti ya tamko hilo imetufikia, nasi tunakufikishia, ambapo Askofu Gwajima anaanza kwa kumnukuu mzungumzaji wa kwenye video mojawapo na kisha kuwataka viongozi wetu kutozimia mioyo kwani kuna jambo ambalo Mungu anataka kulitenda, jambo litakalofurahisha taifa.

"Nataka ujue kwamba mimi niko kama ulivyo lakini upande wa pili." Askofu Gwajima ameeleza, katika ujumbe wake kwa watu hao, ambao amewatanabaisha kama Wafilisti wasiotahiriwa.


Kwa walioshindwa kuisikiliza, basi waweza kuipakua sauti kwa kubofya hapa.

A threat against a nation is a threat against the people. GK inaunga mkono tamko hili na kulaani kila mwenye mkakati wa kuharibu amani ya taifa letu. 

"Ee Rais wa Tanzania usife moyo juu ya maneno haya... Tutasimama na wewe kuanzia mwanzo wa biashara hii, mpaka mwisho wa biashara hii." Ni sehemu ya nukuu tunayomaliza nayo kutoka kwa Askofu Gwajima.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.