UJUMBE KUTOKA KWA MC KING CHAVALA

MC King Chavala
Kwa wanaomfahamu MC King Chavala, wengi wanmtambua kama King of stand up comedy. Lakini pia ni huyuhuyu kijana ambaye ni mhubiri mzuri tu, na pia muimbaji. Leo GK inakuletea nyimbo zake mbili mpya ambazo anakukumbusha mambo kadhaa. La kwanza, kuomba kwa Neno, tofauti na pengine ambavyo siku za hivi karibuni umekuwa ukiongea uongea tu bila hata kujua mstari wa kusimamia. Ujumbe mwingine ni kutukumbusha kwamba Mungu ni Mungu(.)


Pepo hatoki kwa mipayuko wala nini, ila kwa NENO. Kwani maombi ni namba ya kuingia katika ulimwengu wa Roho... Sio lafudhi wala ukali wa maneno yako utakaoondoa pepo. Ila kwa vifungu vya Biblia. "Ukifunga bila kuwa na NENO, hayo ni maandamano ya njaa tu"

Sikiliza wimbo wake hapo chini, ama upakue kwa kubofya hapa


Ujumbe wa pili, hapa King ameamua kwenda kwa miondoko ya rap, lakini anatukumbusha kwamba Mungu ni Mungu. Ni Mungu tangu Adamu hata Elisha, wa mipango zaidi ya ile ya makabrasha. Mungu hawahi wala kuchelewa kujibu maombi ya mtu.


Sikiliza ujumbe (Wewe ni Mungu) hapo chini ama unaweza kuupakua kwa kubofya haoa.


Umepokeaje ujumbe huu? Tungependa kusikia maoni yako.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.