UNACHOPASWA KUFANYA WAKATI UNASUBIRIA MATARAJIO YATOKEE

Faraja Naftal Mndeme,
GK Contributor.

©visacenter

Kila mtu analo taraja fulani kwenye maisha yake,huenda kufikia malengo fulani au kuweza kufikia ndoto zako ambazo umekuwa unazitarajia.Kufika malengo,Tarajio na Ndoto ni mambo ambayo yana mchakato wake.Si mambo ambayo yanatoke siku moja au kutokea ghafla kama Miujiza.Mchakato kwa maana ya kawaida ni hatua moja mpaka nyingine bila kuruka ruka vipengele unavyopaswa kuvipitia kuelekea kwenye malengo,taraja na ndoto zako.

Jamii kubwa ya wanadamu tumekuwa tukitumia muda mwingi kufikiria kufikia ndoto zetu lakini huwa hatutumii muda mwingi kufikiri nini chakufanya wakati tuelekea kwenye ndoto,malengo na matarajio yetu.Kabla ya kufikia ndoto.malengo na matarajio yetu katika utimilifu wake hapa kati kati kuna maisha yanaendelea. Je kipindi hiki cha maisha kinachoendelea kuelekea ndoto zako ni kitu gani Unapaswa kufanya?Au usubiri tu mpaka ufikie ndoto na malengo au matarajio ulio nayo? Ni muhimu kujua unapaswa kufanya kitu gani wakati unasubiri kufikia ndoto,malengo na matarajio ya maisha yako.

1. Ongeza Thamani Yako Kuelekea Kwenye Ndoto,Lengo na Taraja lako.
Iwapo unataka kuwa mtu fulani au unatamani kufanya kitu fulani kwenye maisha yako hakikisha kila siku unaongeza thamani yako kwa kuongeza ujuzi mdogo mdogo kwenye maisha yako kuelekea kufikia lengo,Ndoto na Taraja lako.Mara nyingi unaweza kukuta tumeweza kufikia ndoto,lengo au taraja fulani lakini pamoja na kufikia kilele chake ukijichuguza mwenyewe ndani unajikuta unapwaya fulani.Mfano Unapofikiria kuwa Raisi wa Nchi fulani kabla hujafikia Uko hakikisha Unasoma Vitabu,Makala zinazohusu Uongozi lakini pia hakikisha unajifunza Maadili ya Uongozi ili wakati utakapofika kwenye hio hatua ya kuwa Kiongozi wa Hatua usiwe unapwaya kwa Sehemu kubwa na Matokeo yake unaweza kuwa umefikia hatua hiyo lakini Utaingia gharama nyingine ya kuanza kujifunza taratibu za Uongozi na Mambo kadha wa Kadha .Hakikisha Unaongeza thamani ndogo ndogo kwenye maisha yako ya Kila Siku.

2. Hakikisha Unajua Itifaki(Protocol) za Ndoto,Lengo,Taraja Lako.
Tambua Hakuna jambo jipya ambalo unaweza kulifanya sasa ambalo halikuwahi kufanyika hapo mwanzo,Kila jambo ambalo unalofikiria kulifikia lina taratibu,kanuni na sheria zake.Hakikisha unafwata ,unajua na Unazingatia Itifaki za Ndoto,Lengo na Taraja Lako. Ili Yusufu(Biblia) Kuchaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Misri alipaswa kujua ili Mtu awe Kiongozi alipaswa afanye nini? Ili Mpasa Yusufu anyoe ndevu zote ili aweza kutimiza moja ya Itifaki kuweza kuwa Kiongozi Nchini Misri. Ili Mlazimu Danieli na Wenzake Kusoma Itifaki (Protocol) kwa Muda Wa Miaka Mitatu ili kupata Siku Moja ya Kuweza Kukutana na Mfalme. Hakuna Kitu ambacho hakina Itifaki,hakikisha unajifunza na kuzijua Itifaki za Ndoto,Lengo na Taraja lako ili kuzifikia.Kizazi hiki tumekuwa na kawaida ya Kurahisiha mambo ndio maana muda mwingine mafanikio tunayoyapa hayadumu sababu hatuna Misingi Mizuri na hatupendi kujifunza kwa kina na Umakini.


3. Hakikisha Unajenga Tabia ya Kuwaheshimu Watu Ambao Wamefikia na Kufanikiwa Vitu Ambavyo Vina Muelekeo wa Lengo,Ndoto na Taraja lako.
Ili mtu kufikia Mafanikio fulani yenye kiwango cha juu kuna machozi,jasho na gharama kubwa ambayo ameilipa ambayo Muda mwingine haisemwi aua hauionekani kwa sababu tayari mtu huyo amefikia katika kilele cha Mafanikio fulani.Wahenga Wanasema “Ukitaka Thawabu ya Nabii Muheshimu Nabii”.Nimesikia watu wengi wamekuwa na Tabia ya Kukosoa Mambo kadha wa Kadha kwa Maneno lakini Hao wanaokosoa hawajaanza hata hatua moja.Hakuna Mtu anayeweza kufanikiwa bila Kukosea Sehemu,Makosa ya wengine nay a kwetu ni Sehemu ya Shule ambayo Inatusaidia kufikia Malengo Makubwa Zaidi kuliko pale ya Wale Waliotutangulia Kufikia.Ni Muhimu Iwapo Unapenda kupata Heshima na Kuheshimiwa na Wengine jenga tabia ya kuheshimu Watu wa Kaliba Yako.Jifunze kwao kwa Heshima ,Unyenyekevu na Adabu ndipo Utakapopata Mafanikio Makubwa Zaidi kuelekea kwenye Ndoto,Lengo na taraja lako.Ukitaka kujua Tabia ya Mtu fulani Angalia Anavyo Wazungumzia Wengine.

4. Tafuta Baraza la Washauri.
Hakuna Mtu ambaye amezaliwa anajua Kila Kitu kila Mtu hujifunza kwa Wengine kwa Kusikiliza Mawaidha.Kwenye kila Anguko,kushindwa kuna Ushauri Mbaya Ulitolewa/Hakukuwa na Ushauri Kabisa/Haukusikiliza Ushauri Uliopewa.kwenye Jambo lolote dunia unaloona Mtu alishindwa ujua hakukuwa na Ushauri Sahihi/Haukusikiliza/Hakukua na Ushauri kabisa.Hakikisha kwenye kila hatua ya maisha yako kuelekea kwenye ndoto,lengo,taraja lako Unakua na Baraza la Watu ambao watakushauri kwa Umakini.Wakati unapewa Ushauri hakikisha hautumbukizi Hisia na Mihemko yako Binafsi.Ni Muhimu kutafuta Ushauri kwa Waliokutangulia juu ya kile ambacho wengine wamefanya.Tafuta Watu ambao wana Muelekeo kama Wako na Ukiona hauwezi kuwafikia kwa Namna ya Kawaida Soma Vitabu Vyao ili kujua Mawazo yao na Namna walivyovuka hatua moja kwenda Nyingine kwenye lengo,ndoto na matarajio ambao Walikua nao hapo Mwanzo.

Hitimisho
Ni Muhimu kuhakisha Unajua kipi kinakupasa kufanya wakati upo njia kueleke kwenye Ndoto,Lengo na Taraja Ulilo nalo.Muda Mwingi tumejikuta tumefikia yale tuliyoyatarajia lakini tunafurahia kwa Muda tu na tunaanza hatua nyingine ya kujaza Utupu ambapo unaonekana kwenye kile tulichokifikia wakati kumbe tungeweza kutatua tatizo hilo mapema.Muda Mwingine huwa tunafikia kilele cha Mafanikio yetu lakini ndani tunajisikia Wapweke mithili kana kwamba hatujafikia kile ambacho tulikitarajia na ndipo nafsi zetu zinaanza kutapa tapa kwa kuanza kuanza kufanya vitu vingine ili mradi kujaza ule Upweke uliomo ndani yetu. Hakikisha kila Siku unakuwa na Wakati wa Kujifunza jambo fulani kwenye Maisha yako. Maana yake Usipojifunza jambo jipya leo Maana yake huna tofauti na jana na kama jana haukujifunza basi hauna tofauti na juzi.


E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.