WAISLAMU WATENGENEZA 'UKUTA' WA AMANI KUWALINDA WAYAHUDI NORWAY

Sehemu ya Waislamu wakiwa wameshikana mikono yao.
Jumuiya ya Wayahudi waishio nchini Norway wanaokadiriwa kuwa 1000 sanjari na wadau wengine wa amani walishangazwa na tukio la kundi la Waislamu takribani 1000 kufika kwenye sinagogi siku ya Jumapili na kisha kushikana mikono wakizunguka nyumba hiyo ya ibada jijini Oslo, kama ishara ya amani pamoja na kuchukizwa na mauaji yaliyofanyika nchi jirani ya Denmark wiki kadhaa zilizopita, ambapo Omar Abdel Hamid El-Hussein alifyatulia risasi na kuua watu wawili kwenye mdahalo uliokuwa ukilenga kudumisha uhuru wa kujieleza.

Taifa hilo linalokadiriwa kuwa na Waislamu laki 2 kati ya wananchi milioni 5.2, limeonyesha kuguswa na tukio hilo, ambapo kwa kujitolea, Waislamu takribani 1000 walishikana mikono ili kuonyesha kwamba amani ndio kitu kikubwa kwao, na kwamba licha ya utofauti wa imani zao, bado watasalia kuwa ndugu.

Kinamama wakiwa sehemu ya tukio hilo
Katika tukio hilo ambalo lilivuta hisia za wengi, ilishuhudiwa viongozi wa Wayahudi na Waislamu wakiwa pamoja, jambo ambalo wengi wanaamini litasaidia kuchukulia dini ya Kiislamu kama korofi dhidi ya nyinginezo.

Sauti zilikuwa zikisikika ambapo Waislamu hao waliokuwa wametengeneza duara la amani, (kama walivyolibatiza jina) walikuwa wakiimba kuhusu amani, na kwamba Uislamu ni tofauti na inavyodhaniwa na kuchukuliwa kwamba ni dini ya mauaji.

The Independent.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.