CHAGUO LA GK NI VIWANGO KUTOKA MKOANI, KWAYA ZA DAR ES SALAAM LAZIMA KUJIPANGAKatika chaguo la GK hii leo, tupo jijini Mbeya ambako tumekuchagulia kwaya ya Uinjilisti Forest kutoka usharika wa Kilutheri Forest uliopo jijini humo. Kwaya hii mwezi ulioisha yaani February waliandaa tamasha kubwa la kusifu na kuabudu katika kusherehekea kuadhimisha miaka nane toka kuanzishwa kwake.

Kumbuka awali kwaya hii ilijulikana kama kwaya ya Vijana wakijulikana na album yao iliyofanya vizuri iitwayo 'Tunaishi' ila kutokana na mabadiliko ya kikatiba kuhusu umri na mamno mengine katika kanisa basi kwaya ya vijana ikaundwa upya na wao wakichukua jina la Uinilisti. Leo tumekuchagulia wimbo 'Yesu ni Ngome yangu' ambao waliimba live siku hiyo ya tamasha ukiongozwa na Dkt Tuntufye Mwamugobole ambaye awapo jijini Dar es salaam huimba katika kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ambako alianzisha pambio la 'Ndani ya Safina'.

Kuna sababu nyingi ambazo zimefanya tukauchagua wimbo huu leo kwanza ni ujumbe  lakini pili ni ubora wa uimbaji ulionyeshwa na kwaya husika ingawa video ilirekodiwa kwa hali ya kawaida tu lakini unaweza kusikia sauti vyema na muziki mzuri huku shangwe na nderemo zikiwa zimechangamsha siku hiyo katika usharika huo wa Forest huku kwaya alikwa walikuwa Tumaini Shangilieni Kwaya kutoka Arusha. Kama kwaya toka mikoani zinaweza kumwimbia Mungu kwa viwango namna hii, ni matumaini yetu kwaya zilizopo jijini Dar es salaam kuna kitu cha kujifunza maana Mungu wetu anatakiwa kuimbiwa kwa viwango vya hali ya juu.

Tunakutakia baraka za Mungu utazamapo wimbo huu. Barikiwa

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.