DALILI CHACHE KWAMBA UKO KATIKA MUELEKEO MZURI

Na Faraja Naftal Mndeme.
GK Contributor.


1. UNATOA MSAADA KWA WENGINE.

Namna dunia yetu ilivyo leo na mambo yanavyokwenda ni ngumu sana kutumia muda wako kuishughulisha na mambo ya mtu mwingine wakati  ya kwako yanakuongoja.Lakini zaidi ya yeyote tunatambua hakuna mtu anayeweza kuishi kwa kijtegemee mwenyewe kwenye kila jambo kwenye maisha yetu kama wanadamu.Mifumo ya Uchumi,Elimu,Siasa na Ya Kijamii mara nyingi haitoi mwanya wa kuweza kuwasaidia wengine kwa ukaribu haswa katika dunia yetu ya Mitandao ya Kijamii.Ni Muhimu kuwasaidia wengine si kwa sababu wao wanahitaji msaada wako bali ni moja ya akiba unayojiwekeze katika siku zako za usoni pindi na wewe utakapohitaji msaada wao.

2.  KUTAMBUA CHANGAMOTO NI SEHEMU YA MAISHA.

Hakuna mtu anaishi bila changamoto lakini kuna wengine wanafanikiwa kuvuka kwenye changamoto kwa urahisi kwa sababu ya aina ya mtazamo juu ya changamoto wanazopitia maishani mwao.Muda mwingine vile unavyozitazama changamoto zinazokuzunguka ni changamoto pia.Mtu ambaye mwenye ufahamu sahihi huwekeza muda wake katika kutatua changamoto zake maana anatambua changamoto ni sehemu ya mafanikio kwenye maisha yake.Changamoto hutusaidia kukua katika mitazamo mbali mbali maishani mwetu na kuweza kutusogeza katika mafanikio tunayoyahitaji.

3. KUTOKUWA MLALAMISHI WA MAMBO.

Mara nyingi kulalamiki hakukusaidii kutatua tatizo bali kunasaidia kukuongezea mzigo wa msongo wa mawazo kutoka hatua moja kwenda nyingine.Kulalamika kupita kiasi ni dalili kwamba bado hakuna ukomavu kwenye utashi wako na ni dalili ya kwamba hauko kwenye muelekeo bora.Mtu mwenye muelekeo mzuru hutumia muda wake kufikiria na kutenda kile anachofikiria kwamba ni sahihi na kinaweza kumvusha kutoka hatua moja ya maisha yake kwenda nyingine.Ulalamishi wa jambo lolote ni dalili ya kwamba una uoga wa fikra na kimawazo na pia kuna aina fulani ya ukomavu unakosekana kwenye tamia yako.Ni Muhimu kupunguza Ulalamishi usiokuwa na maana na kuwekeza muda wako kwenye kutafuta suluhisho ya kile kinachokukabili.

4.UNAFURAHIA MAFANIKIO YA WENGINE.

Kila mtu kwenye maisha ana aina fulani ya mafanikio amabayo mwingine hata.Unapoweza kufurahia aina ya mafanikio ambayo mwingine ameyapata ni dalili kwamba kuna ukomavu mkubwa kwenye akili yako na uko katika ueleko sahihi.Wivu,Chuki,Husuda,Kijicho ni dalili ya kwamba ukomavu wako wa kitabia,kiakili na kifikra ni mdogo.Muda mwingie namna nzuri ya kufanikiwa kwenye maisha ni kutambua na kufurahia mafanikio yaw engine maana kupitia wao unaweza kujifunza mambo kadha wa kadha kutoka kwao.Chuki hukujengea kiburi,majuto na hasira ambazo hazina msingi na mashiko yoyote na zaidi ya yote unajitengenezea mazingira ya kuharibu nafsi yako kwa kuilisha sumu mbaya ambapo itakuchukua muda kuitoa na isipotoka inaweza kukupelekea mauti.

5. UNAFURAHIA MAFANIKIO YAKO.

Mara nyingi tumetumia muda mwingine kujilinganisha na wengine kama ishara ya kwamba hatujafanikiwa lakini tunasahau hata kile ulichokipata ni kufanikiwa maana kuna mtu anafikiria kufika hatua kama yako lakini hajafanikiwa.Kufurahia kile unalichonacho ni hatua thabiti ya kuonyesha una shukrani kwenye kile ulichopatiwa na pia unaweza kuongezewa kingine.Ni vigumu sana kumapatia mtu kitu kingine wakati kila cha kwanza ulichompatia anakilalamikia kupita maeleo.Mafanikio yako ya leo ni jitihada zako za jana,Furahia jitihada zako za jana kwa kuwekeza leo ili kesho yako iwe bora kuliko leo yako.Dunia imeeumbwa kwa mfumo wa kupata na kushukuru,Iwapo huna furaha na kile ulichonacho leo ni ngumu kufurahia kile utakachopata kesho na unaweza ukawa unajitengenezea misongo   ya mawazo isiyokuwa na ulazima.Jifunze kufrahia mafanikio yako katika kila hatua maana Hayo ni Matunda ya jitihada zako na ni nzuri kwa afya ya akili yako pia.

E-mail:naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.