ENOCK MWETA: SURA MPYA KWENYE UIMBAJI BINAFSI

Enock Mweta akihudumu
‘Report’ ndio jina la albamu ya kwanza ya muimbaji wa nyimbo za injili, Enock Mweta, ambaye licha ya kuhudumu kwenye kwaya ya Dar es Salaam Gospel Choir iliyopo Kurasini katika kanisa la Free Pentecoste Church of Tanzania, imefika wakati muafaka wa kutoka kama solo artist kwa kurekodi nyimbo zake ambapo anatarajia kuachia album hiyo mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Pamoja na Dar es Salaam Gospel Choir, Enock pia ameshawahi kuhudumu na kwaya zingine za Tuliza Moyo na Joy Singers za FPCT korogwe, mkoani Tanga.

Album hiyo aliyofanya kwa ushirikiano na msanii mkongwe kwenye tasnia ya injili Jackson Bent inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni ikiwa na nyimbo kama Unywe Maji, Report, Mfalme, Usilalamike, Pendo Lako, Mungu Muweza, na Niko na Yesu.

Enock ambaye ni mume wa mke mmoja, Angel, naeleza zaidi kuwa nyimbo hizo ni mchanganyiko lakini nyingi ni za sifa katika album hiyo kwani yeye binafsi anapenda sana nyimbo za kumsifu Mungu.
Enock na mkewe, Angel.
Pamoja na kuomba kupokelewa vizuri na Watanzania, anaamini kwamba kupitia album hiyo watu wengi watabarikiwa na watafurahia. Halikadhalika ameomba waimbaji wa injili kuendelea kujenga umoja, upendo na ushirikiano katika kuifanya kazi ya Mungu.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.