GWIJI WA MUZIKI WA INJILI DUNIANI KUREKODI LIVE DVD NCHINI AFRIKA YA KUSINI MWAKA HUU

Mchungaji na mwimbaji Donnie McClurkin
Gwiji wa muziki wa injili duniani mchungaji Donnie McClurkin anatarajiwa kurekodi DVD yake mpya baadaye mwaka huu nchini Afrika ya kusini. Mwimbaji huyo ambaye amefanyika baraka kwa watu wengi tayari amewasili nchini Afrika ya kusini kwaajili ya maandalizi ya dvd hiyo ambayo inatarajiwa kuwashirikisha waimbaji wengi wa Afrika ya kusini.

Aidha uamuzi wa nguli huyo kurekodi Afrika ya kusini inawezekana ikawa nafasi nzuri ya kujitangaza duniani kwa waimbaji wa nchini humo ambao wanatarajiwa kushirikishwa. Mpaka sasa mwimbaji wa zamani wa Joyous Celebration mwanadada Mahalia Buchanan au mwite Hally ni mmoja kati ya waimbaji wanaonekana watakaoshirikishwa na mchungaji Donnie ambapo wakati alipoanza safari yake kuelekea Afrika ya kusini majuzi kupitia ukurasa wake wa instagram Donnie alitaja jina la Mahalia na Jonathan kuwa  anahamu ya kukutana nao tena pamoja na kutoa tangazo kwa waimbaji,wanamuziki na wachezaji watakaopenda kushirikishwa katika DVD hiyo angependa kukutana nao wiki hii mjini CapeTown.

Mahalia Buchanan nyota wa zamani wa Joyous Celebration
Ikimbukwe kwamba Mahalia aliweza kumbariki mchungaji Donnie pale alipoimba moja ya wimbo wake kwa kiwango cha hali ya juu, aidha mwanadada huyo hakumshangaza Donnie peke yake bali pia James Fortune alipokwenda Afrika ya kusini, Mahalia aliimba wimbo wa Tasha Cobbs kwa kiwango cha juu hadi kumfanya mwanamuziki huyo kuweka kipande cha Mahalia akiimba wimbo huo katika ukurasa wake wa Instagram na kumtagi Tasha Cobbs ambaye naye alionekana kubarikiwa na uimbaji wa Mahalia ambaye pia anatarajia kurekodi DVD yake ya kwanza live mwezi june mwaka huu.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.