HATUA TATU MUHIMU ZA UKUAJI KWENYE JAMBO LOLOTE LILE

Na Faraja Naftal Mndeme


DEPENDENT (UTEGEMEZI).
Kitu chochote kuanza uhai huanzia sehemu fulani ya utegemezi. Wanadamu wote ili kuanza kuishi tulitegemea tumbo la mama kutubeba kwa miezi tisa kabla ya kuanza kujitegemea kwa mambo kadha wa kadha. Na hata baada ya kuzaliwa tuliwahitaji wazazi kutukuza, kutulisha na kutuongoza kabla ya kuanza kujitegemea. Tuliwategemea wazazi kutuambia maneno mazuri ili tuweze kujisikia vizuri. Tuliwategemea wazazi/walezi katika kila namna kuanzia kiuchumi, kijamii, kisiasa na kihisia ili kuweza kujiendesha kwenye jambo lolote lile. Iwapo wazazi/walezi hawakuwepo pamoja na sisi kwenye jambo lolote lile tulilaumu au kujisikia vibaya sana. Maisha yetu yote yalitegemea uwepo wao ili sisi tuweze kuishi vyema. Na pale wasipokuwepo tuliathirika kwa namna moja au nyingine.

INDEPENDENT (KUJITEGEMEA)
Hii ni hatua muhimu ya pili baada ya kutoka kwenye kuwategemea walezi/wazazi kwenye mambo mengi ya maisha yetu. Inapofika swala la kujitegemea ni kama mtoto anapoweza kusimama mwenyewe na kuweza kukimbia au kutembea bila kushikiliwa au msaada wa kitu chochote. Maisha yetu yanakuwa ya kwetu wenyewe na hapa ndipo tunajiendesha wenyewe kwenye mambo kadha wa kadha kiuchumi, kisiasa, kijamii na kihisia. Hatua hii ni muhimu sana ingawa baadhi yetu tunafikiri kujetegemea ni kuongea au kuweza kujielezea tu. Moja ya dalili ya mtu ambaye bado hajafikia kujitegemea utamsikia “Yaani Kama Sio Mtu fulani Nisingekuwa Hivi Leo” Kama baba angekuwepo nisingepata mateso haya” Yaani kama si kitu fulani…” Yaani design hii ya mtu anategemea mtu mwingine afanye kitu fulani yeye ajisikie vizuri, "Yaani boyfriend wangu ananiudhi kila saa yaani sina raha”... Ukiona maamuzi ya mtu mwingine ndio yaamue hisia zako, mood zako, hali yako ya kiuchumi… Ujue bado wewe ni dependent (Mtegemezi)

INTERDEPENDENT (KUTEGEMEANA)
Hii ni hatua ya juu ya ukuaji kwenye jamii ya wanadamu. Yaani mtu baada ya kuweza kujitegemea ndipo mnaanza kutegemeana. Hapa kuna tatizo kubwa, sanasana utakuta mtu ametoka kuwa dependant (Mtegemezi) kihisia, kiuchumi na kijamii n.k then anataka kuanza kutegemeana na mtu mwingine. Umeshawahi kujiuliza kwanini mahusiano mengi yakivunjika mmoja anaathirika sana kuliko mwingine? Hisia zozote ambazo zilikuwa zikimtegema mwingine afanye kitu ndio wewe ufanye au ujisikie vizuri ujue hilo ni tatizo. Kabla haujaingia kwenye mahusiano hakikisha unaweza kujitegemea kihisia. Usikurupuke tu kuingia. Utasikia mtu anasema girlfriend/rafiki/mchungaji wangu hanifanyi kuwa na furaha. Ina maana wewe hisia zako zinaamuliwa kulingana na namna mwingine anavyojisikia. Vipi mtu huyo siku hiyo akiwa mood less au akiwa anaumwa?...  Jifunze kujitegemea kwanza… Don’t let external factors kuifluence character yako halisi. Character yako ndio inaamua nini kifuate na kipi kisifuate. Ukiona unakuwa influenced na external factors juu ya jambo fulani basi tambua kazi Ipo…Wewe bado ni DEPENDENT (MTEGEMEZI) na sio INDEPENDENT (KUJITEGEMEA)… Bosi wako kazini ndio anaamua siku yako iwe nzuri au mbaya? Kweli Kabisa... Unalalamika. .Je hapo tatizo ni bosi au wewe ndio tatizo? Ukiona maamuzi ya mtu mwingine ndio yanaamua kitu gani kifuate kwenye maisha yako tambua kwamba bado wewe upo hatua namba moja yaani bado ni mtegemezi.

E-mail: naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless Y’All

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.